Martha Mwaipaja: Jaribu Kwa Mtu Lyrics na Mafunzo

Posted by:

|

On:

|

Hapa utapata Jaribu Kwa Mtu Lyrics by Martha Mwaipaja. Mwishoni utapata mafunzo na maandiko ya biblia ya kukutia moyo.

Martha Mwaipaja Jaribu Kwa Mtu Lyrics

Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi,

Ila ni kikombe tuu lazima akinywe.

Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu,

Ila ni wakati tuu ambao ni lazima apitie.

Usimuone mtu anapita kwenye jaribu anavumilia,

Kwa sababu ni wakati wake.

Maumivu aliyonayo hawezi mpa mtu,

Ananyamaza kwa sababu ni kikombe chake.

Hakuna aliewahi omba kwa Mungu apitie yale anayoyapitia,

Hakuna aliesema na Mungu yampate yaleyale yanayompata.

Jaribu lingeondolewa kwa kuomba sana,

Wote tungeomba tusipite kwenye Jaribu.

Jaribu lingekwepeka kwa kufunga sana,

Ndugu yangu wengi tungefunga tusipite kwenye jaribu.

Mtu mwenye Jaribu hajaomba kwa Mungu,

Ni wakati tuu anapitia.

Mtu mwenye pito hajaomba kwa Mungu,

Ni wakati tuu ni wakati anapitia.

Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi,

Ila ni kikombe tuu lazima akinywe.

Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu,

Ila ni wakati tuu ambao ni lazima apitie.

Kulikuwa na Ayubu aliemcha Mungu..Mungu mwenyewe alijivunia Ayubu,

Ayubu hakujua kwamba ipo siku moja itafika atapita kwenye jaribu.

Ayubu hakujua kwamba ipo siku moja itafika atapita kwenye jaribu.

Siku Moja Mungu akakutana na shetani akasema shetani wewe umetoka wapi?

Shetani akajibu nimetoka duniani nikizunguka zunguka huku na kule.

Mungu akasema Umemwona mtu wangu hapanaa mtu mwema kama Ayubu.

Shetani akasema ni kwa sababu umemzingira pande zotee huyo.

Jaribu kutoa kila kitu uone kama Ayubu hatakutenda dhambi.

Ayubu akaanza kupitishwa kwenye taabu zote,

Kwa sababu Mungu alijivunia Ayubu.

Ayubu akaanza kupitishwa kwenye mateso yote,

Ni kwa sababu Mungu alijivunia Ayubu.

Ayubu hakujua kwamba Mungu wa mbinguni anajivunia yeye.

Alipitia mengi, alisongwa na mengi,

Yote ni kwa sababu Mungu alijivunia Ayubu.

Alisongwa na mengii alipitia Mengi,

Ayubu akasema pamoja na yote nitaishi.

Ndipo nimejua kumbe yote yanipatayo mimi ni kwa muda,

Sijatenda dhambi, hujatenda dhambi,

Ni wakati tuu lazima tupitie.

Usimuone mtu analia sasa,

Ni Mungu anajivunia hayo.

Kumbe mengi yanatukuta sisi hatujui,

Lakini Mungu anajivunia sisi.

Anajua mwanzo anajua mwisho,

Ni baba anajivunia sisi.

Unapitia mengii unasongwa na mengi,

Kumbe Mungu anajivunia wewe.

Tulia kwa Mungu tulia kwa baba,

Ili mwenyewe ajitukuze kwako.

Kweli tunachoka kweli tunashindwa,

Lakini Mungu anajivunia sisi.

Hatuwezi kuwa washindi hatuwezi kung’aa sana,

Lazima Mungu ajivunie.

Hatuwezi kuendelea hatuwezi kuvuka ng’ambo,

Lazima tupitie haya.

Jaribu lako ni wakati tuu Mungu anajivunia,

Jaribu lako ni wakati tuu ni wakati unapitia.

Jaribu kwa mtu si kwamba ni mtenda dhambi,

Ila ni kikombe tuu lazima akinywe.

Jaribu kwa mtu si kwamba kakosa kwa Mungu,

Ila ni wakati tuu ambao ni lazima apitie.

Mafunzo kutoka kwa huu wimbo

Vumilia nyakati za majaribu

Kila mtu anapitia majaribu na lazima avumilie, changamoto za maisha haziepukiki. Jambo kuu ni kuvumilia na kuamini kuwa majaribu yanapita kwa wakati.

Yakobo 1:2-3: Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu.

Kukabili changamoto kwa imani

Majaribu si ishara ya kosa bali ni sehemu ya lazima ya safari ya mtu. Tumaini katika wakati wa Mungu na pitia changamoto kwa imani.

1 Petro 1:6-7: Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka, majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.

Omba na ufunge

Maneno haya yanapendekeza kwamba ili majaribu yaepukwe, watu wanapaswa kuomba na kufunga ili kuyaepuka.

Yoeli 2:12-13: “Lakini hata sasa,” nasema mimi Mwenyezi-Mungu, “Nirudieni kwa moyo wote, kwa kufunga, kulia na kuomboleza. Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni bali nirudieni kwa moyo wa toba.” Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; yeye amejaa neema na huruma; hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili; daima yu tayari kuacha kuadhibu.”

Mungu anapendezwa na watoto wake

Sawa na simulizi la Ayubu katika Biblia, ambapo Shetani anajaribu imani ya Ayubu, Mungu anajivunia wale wanaobaki waaminifu hata wanapokabili majaribu. Wimbo huu unasisitiza kwamba Mungu anajivunia watu kama Ayubu.

2 Wakorintho 4:17: Taabu tunayopata ni kidogo, tena ya muda tu; lakini itatupatia utukufu upitao matazamio yote, utukufu ambao hauna mwisho.

Majaribio ni ya muda

Kubali kwamba kila kitu kilichotokea, kiwe kizuri au kibaya, ni cha muda tu. Majaribu ni nyakati za wakati, na kuyastahimili ni ushuhuda wa nguvu na imani ya mtu.

1 Wakorintho 10:13: Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.