Wimbo huu wa kizalendo “Wimbo wa historia” uliandikwa na Enock Ondego miaka ya 1970. Inafafanua majaribio ya watu weusi katika kupigania uhuru kutoka kwa Waingereza. Wimbo huu unajulikana haswa kwa sauti yake ya hisia katika kuelezea hadithi za Kapenguria Six; hasa Mzee Jomo Kenyatta.
Leyla Mohamed ameipatia mwonekano mpya na uimbaji ulioboreshwa ambao umefadhiliwa na ” Permanent Presidential Music Commission”. Hapa ni wimbo wa historia lyrics.
Wimbo wa historia lyrics
Wimbo huu uliimbwa historia
watu wote mnaombwa msikize kwa makini.
Ilikawa October hamsini na mbili
watu wote tulisikia Kenyatta ameshikwa,
hakushikwa kenyatta pekee yake lakini
alishikwa na mabingwa wa uhuru
(woo woo wooooo)
Ilikua kilio nchini kenya
watu wote tuliona huzuni mwingi sana,
wakina baba akina mama na watoto
wote walilia machozi wakisema,
woooi woooooi wooi, tunataka kenyatta aachiliwe.
Baba wa taifa alipotoka gerezani
aliwakuta wajumbe wetu wametengana vibaya sana.
Aliongoza wajumbe mpaka ulaya
kufika huko alipigwa na mayai yaliyooza.
Mzee wetu hakujali alishinda
na kurudi na katiba ya nchi yetu hapa kenya,
mzee wetu alituomba tusahau yaliyopita
badala yake tuijenge nchi yetu.
Ooh asante baba wetu,
wengi wee asante baba wetu.