Fahali ni dume la ng’ombe.
Kinyume cha fahali
Neno kinyume linaweza kufafanuliwa kuwa neno linaloonyesha maana kinyume na maana ya neno fulani.
Kinyume cha neno “fahali” ni “mtamba, mfarika au dachia”, ambayo ni jinsia tofauti ya “fahali”. Fahali pia hujulikana kama ng’ombe wa kiume, na wana nguvu zaidi kuliko ng’ombe wa kike, na pia ana mifupa minene.
Mtamba ni mnyama kike aghalabu ng’ombe ambaye bado hajazaa.
Mfarika ni mnyama hususan mbuzi, ng’ombe au ngamia aliyekomaa lakini bado hajazaa.
Dachia ni mnyama yeyote jike ambaye amekomaa na anaweza kuzaa au kupata mtoto.