Tabasamu ni kuonyesha hali ya kutaka kucheka bila ya kutoa sauti.
Mfano: Juma hutabasamu kila anaponiona.
Kinyume cha tabasamu
Kinyume cha tabasamu ni: mnuno, nuna fura au tuna.
Nuna ni kukataa au susa kuongea baadha ya kuudhiwa au kukerwa na jambo au mtu fulani.
Mnuno ni hali ya kuchukia, ukaaji kimya baada ya kuchukizwa, tendo la kununa.
Fura na tuna ni kuwa na hasira.
Kinyume cha nuna
Kinyume cha neno nuna ni tabasamu.