Mistari ya toba katika biblia

Toba ni kujisikia huzuni kuhusu dhambi yako na kuamua kubadilika. Wale wanaotubu hukataa dhambi na kutambua kwamba wanamhitaji Yesu ili waokolewe. Hizi hapa ni mistari ya toba katika biblia za kukusaidia kutubu dhambi zako.

Mistari ya toba katika biblia

Matendo 3:19 BHN

Basi, tubuni, mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu.

Luka 13:3 SRUVDC

Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

2 Mambo ya Nyakati 7:14 BHN

kama watu hao wangu wakijinyenyekesha, wakasali, wakanitafuta na kuacha njia zao mbaya, basi, mimi nitawasikiliza kutoka juu mbinguni; nitawasamehe dhambi yao na kuistawisha nchi yao.

Matendo 17:30 BHN

Mungu alifanya kana kwamba haoni nyakati zile watu walipokuwa wajinga. Lakini sasa, anaamuru watu wote kila mahali watubu.

Mathayo 4:17 SRUV

Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Ezekieli 18:30 BHN

“Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema hivi: Nitawahukumu nyinyi Waisraeli, kila mmoja wenu, kulingana na mwenendo wake. Tubuni na kuachana na makosa yenu, yasije yakawaangamiza.

Marko 1:15 BHN

“Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema!”

Matendo 2:38 BHN

Petro akajibu, “Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile ahadi ya Roho Mtakatifu.

Ufunuo 3:19 BHN

Mimi ndiye mwenye kumwonya na kumrudi yeyote ninayempenda. Kwa hiyo uwe na bidii na kutubu.

Yakobo 4:8-10 BHN

8 Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki! 9 Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na furaha yenu iwe huzuni kubwa. 10 Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni.

Matendo 26:20 BHN

Ila nilianza kuhubiri kwanza kwa watu wa Damasko, halafu kwa wale wa Yerusalemu na nchi yote ya Yudea, na pia kwa watu wa mataifa mengine. Niliwahimiza wamgeukie Mungu na kuonesha kwa vitendo kwamba wamebadilisha mioyo yao.

Luka 15:10 BHN

Kadhalika nawaambieni, ndivyo watakavyofurahi malaika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja anayetubu.”

2 Petro 3:9 SRUV

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.

Zaburi 51:17 SRUV

Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.

Mathayo 3:8 BHN

Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu.

Yoeli 2:12-13 BHN

“Lakini hata sasa,” nasema mimi Mwenyezi-Mungu, “Nirudieni kwa moyo wote, kwa kufunga, kulia na kuomboleza. Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni bali nirudieni kwa moyo wa toba.” Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; yeye amejaa neema na huruma; hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili; daima yu tayari kuacha kuadhibu.

1 Yohana 1:9 NEN

Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.

Isaya 30:15 BHN

Bwana Mungu, Mtakatifu wa Israeli, asema: “Mkinirudia na kutulia mtaokolewa; kwa utulivu na kunitumainia mtapata nguvu.” Lakini nyinyi hamkutaka.

Luka 24:46-48 – Bibilia Takatifu

46 aka waambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 47 Habari hii ya wokovu itatangazwa kwanza Yerusalemu hadi kwa mataifa yote, kwamba: kuna msamaha wa dhambi kwa wote watakaotubu na kunigeukia mimi.

1 Timotheo 2:4 BHN

ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli.

Warumi 2:4 NEN

Au waudharau wingi wa wema, ustahimili na uvumilivu wake, bila kujua kuwa wema wa Mungu wakuelekeza kwenye toba?

Ufunuo 2:5 BHN

Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukatubu na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa mahali pake.

Matendo 11:18 BHN

Waliposikia hayo, waliacha ubishi, wakamtukuza Mungu wakisema, “Mungu amewapa watu wa mataifa mengine nafasi ya kutubu wapate uhai!”

Mathayo 9:13 BHN

Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: ‘Nataka huruma, wala si tambiko.’ Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.”

Mithali 28:13 SRUV

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

2 Wakorintho 7:9-10 BHN

Sasa nafurahi, si kwa sababu mmehuzunika, ila kwa kuwa huzuni yenu imewafanya mbadili nia zenu na kutubu. Mmehuzunishwa kadiri ya mpango wa Mungu, na kwa sababu hiyo hatukuwadhuru nyinyi kwa vyovyote. Kuwa na huzuni jinsi atakavyo Mungu husababisha badiliko la moyo, badiliko lenye kuleta wokovu; hivyo hakuna sababu ya kujuta. Lakini huzuni ya kidunia huleta kifo.

Luka 5:32-39 – Bibilia Takatifu

Sikuja kwa ajili ya wenye haki bali nimekuja kuwaita wenye dhambi ili watubu.”

Ezekieli 33:11 BHN

Basi, waambie: Kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu naapa kwamba, mimi sikifurahii kifo cha mtu mwovu, bali napenda mtu mwovu aachane na mwenendo wake mbaya, apate kuishi. Tubuni, achaneni na mwenendo wenu mbaya, enyi Waisraeli! Kwa nini mwataka kufa?

Ufunuo 2:16 BHN

Basi, tubu. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.

Matendo 5:31 SRUV

Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kulia, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.

Related Posts