Chimba ni:
Fukua ardhi.
Mfano: Kabla nyumba haijajengwa ni lazima kuchimba msingi.
Soma kwa bidi.
Takia mtu afikwe na mkasa.
Mfano: Chimba mtu.
Fuatafuata mtu hasa kazini.
Kinyume cha chimba
Hapa ni vinyume vha chimba kulingana na muktadha unaokusudia:
Kinyume cha chimba (fukua ardhi) ni fukia, funika.
Fukia ni kujaza shimo kwa udongo, ficha ardhini.
Funika ni ziba kitu ili kisiweze kuonekana.
Neno chimbua lina maana mbili:
- Chimba ardhi na fukua udongo.
- Saka asili ya kitu au jambo.
Katika huu muktadha kinyume cha chimba hakiwezi kuwa chimbua kwa sababu maana ya chimba na chimbua ni sawa.
Kinyume cha chimba mtu ni chimbua.
Katika huu muktadha kinyume cha chimba(mtu) ni chimbua. Unachimbua mtu ili asifikwe na mkasa.