Chombezo – Jamani b…
 
Notifications
Clear all

Chombezo – Jamani binamu! (Sehemu ya kwanza)


Posts: 64
Admin
Topic starter
(@aislingbeatha)
Member
Joined: 1 year ago

Ilikuwa mwaka 2008 nilipomaliza kidato cha nne,lakini matokeo yangu hayakuwa mazuri sana kwani sikuweza kupata credit ambazo zingeweza kunipeleka form five ivyo nilibaki nyumbani kusaidia kazi za nyumbani kama kwenda shamba kipindi cha kilimo kinapofika.

Sio siri maisha ya kijijini yalinichosha sana kwani yalinifanya nizeeke mapema sana wakati sikuwa hata na umri mkubwa ndo kwanza nilikuwa na umri wa miaka kumi na tisa,niliyachukia sana maisha hayo pili niliwaonea wivu wezangu waliobahatika kufahulu na kuingia kidato cha tano

Siku moja nikiwa nyumbani alikuja rafiki yangu mmoja tuliyekuwa nae kijijini ila kwa sasa yeye anaishi jijini Dar es salaam,sio siri alipendeza sana kwani alivaa nguo zilizomuonyesha ametoka mjini,moyoni nilimuonea wivu sana kwani na mimi nilitamani kuwa kama yeye,alinipa michapo mingi sana ya maisha ya Dar es salaam hapo na mimi ndo alinipa mzuka wa kutaka kufika katika jiji hilo ili nikajionee aliyoniambia.

“Thomas”aliniita mshikaji wangu aliyekuwa anajulikana kwa jina la Anthony

“naam”niliitika

“Dar es salaam kuna raha sana,kuna wanawake wazuri,kuna sehemu nyingi sana za kutembelea kama beach,club na nyinginezo pia kuna majumba makubwa na magari ya kila aina”Anthony aliongea kwa msisitizo mkubwa sana

“Natamani niende ila nyumbani hawawezi kuniruhusu japo nina mjomba wangu anaishi huko”niliongea

“Kweli wewe endelea kukaa kijijini uchakae na jembe”aliongea kwa kejeli

Tuliongea mengi sana lakini kichwani nilikuwa nawaza kama na mimi siku moja nitafika jiji la Dar es salaam nikajionee mambo yote niliyohadithiwa na rafiki yangu,alipomaliza kunipigia story zake akaniaga na kuondoka zake huku akiniacha nikimuonea wivu kwa jinsi alivyopendeza.

Ilipita miezi miwili nikiendelea na shughuli za kilimo kijijini huku nikiwaza ni jinsi gani naweza kuenda Dar es salaam ila nilikuwa naofia kuwaambia wazazi kwani nilikuwa najua watanikatalia.

Siku moja nikiwa nyumbani tulipata mgeni kutoka Dar es salaam,alikuwa ni mjomba pamoja na shangazi walikuja kututembelea kijijini sio siri nilifurahi kwani nilijua naweza kupata japo nafasi ya kuelekea huko.

Jioni ilifika tukakusanyika pamoja na kubadilishana mawazo huku nikiwa na shauku la kutaka kujua mengi kuhusu jiji la dar es salaam, kama mjomba alikuwa kwenye mawazo yangu

“uncle unaonaje tukienda wote Dar es salaam nataka ukawajue ndugu zako?”mjomba alisema

Nilitamani kuruka ruka kwani nilikuwa nataka kusikia neno kama lile, sikuamini kama mjomba alikuwa kwenye mawazo yangu.

“Kweli tena atatusaidia mambo mengi sana pale nyumbani kwani shughuli zilikuwa nyingi sana”alisema shangazi.

“Jamani na kazi za shamba nani atafanya?”aliuliza baba

Sio siri nilianza kukasirika kwani baba alianza kuleta unoko,ila mjomba akamshawishi baba mpaka akakubali,niliambiwa kesho nijiandae kwaajili ya safari ya kesho kutwa,sio siri nilifurahi sana mpaka usiku huo sikuweza kupata usingizi kwani nilikuwa nasubiri kwa hamu sana safari ya kuenda Dar es salaam

Asubuhi niliamka na kufanya shughuli za pale nyumbani,nilipomaliza nikaenda kufua nguo zangu ambazo niliziona pamba sana kwa wakati huo,nilipomaliza kufua nikaanza kuzunguka mtaani kuwaaga watu hasa niliokuwa nawafahamu,kichwani nilijihisi fahari sana kwani kuenda Dar es salaam ilikuwa jambo la heri sana kwangu.

Nilirudi nyumbani ili niweze kujiandaa kwa safari ya kesho yake,nyumbani niliwakuta akina mjomba wamekaa nje wakipiga story nami nikakaa kujumuika nao, tulipiga story mpaka saa tatu,niliwaaga nakwenda kulala ili kesho niamke mapema kwaajili ya safari, lakini sikuweza kulala kwani nilikuwa na kihoro.

Nilikuja kushtuka usingizini ilikuwa saa kumi na moja nikainuka na kuanza kujiandaa, wakati najiandaa kumbe nao akina mjomba walikuwa wameshaamka na ndo walikuwa wanajiandaa.

Walipomaliza kujiandaa wakanipitia chumbani kwangu ili tuweze kuondoka,muda wote huo nilikuwa siamini kama naenda Dar es salaam,nilitoka na kuanza kuwaaga wazazi japo ilikuwa ni majonzi kuachana na wazazi wangu lakini ilibidi nifanye ivyo.

Tulipanda katika gari la mjomba kwani mjomba alikuja na gari lake, mimi nilikaa seat ya nyuma mjomba na shangazi walikaa seat ya mbele huku mjomba akiwa ndo dereva, niliwapungia wazazi mkono kwa ishara ya kuwaaga kwani ndo nilikuwa nakiaga kijiji cha Kwasunga wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Mjomba aliwasha gari na kuanza safari ya kuelekea Dar es salaam njiani nilikuwa nashangaa maeneo tuliyokuwa tunapita huku nikifurahia kwani ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kusafiri kwa umbali mrefu.

Tulitumia muda wa masaa matano mpaka kufika jijini dar es salaam, tulipofika maeneo ya Baruti gari lilikunja mkono wa kulia lilitembea kwa dakika chache mpaka kufika nje ya nyumba moja ya kifahari, mjomba alipiga honi hazikupita dakika nyingi geti likafunguliwa na mtu ambaye nilikuja kujua ndio mlinzi wa nyumba hile.

Tuliingia ndani ya nyumba hile na kushuka kwenye gari huku nikiwa naishangaa nyumba hile jinsi ilivyokuwa nzuri,ghafla walitoka ndani wasichana wawili ambao wakiwa na sura za tabasamu wakaenda kumkumbatia mjomba na shangazi.

Niliwaangalia watoto wale na kugundua kwamba walikuwa watoto wa mjomba kwani walifanana sana na shangazi, mmoja alikuwa mrefu kuliko mwenzake japo sio sana kwani walikuwa wanakaribiana,walipomaliza kusalimiana wakanigeukia na kunisalimia huku wakinishika mkono. (Itaendelea katika sehemu ya pili)