What does the Bible say about sin?
Mithali 28:13 ESV
Afichaye makosa yake hatafanikiwa, bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Mwanzo 4:7 BHN
Je, ukitenda vyema hutakubaliwa? Na usipotenda vyema, basi, dhambi inakuvizia mlangoni; inakutamani, lakini unapaswa kuishinda.”
Yakobo 1:15 SW
Kisha tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
2 Timotheo 3:1-5
Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. Watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu; watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema; watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo.
Mathayo 5:48 SW
Basi ninyi mnapaswa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
1 Yohana 3:6-10
6 Hakuna mtu anayedumu ndani ya Kristo ambaye anatenda dhambi; na mtu ye yote anayetenda dhambi, huyo hajapata kumwona Kristo wala kumjua.
7 Watoto wadogo, mtu asije akawadanganya. Kila atendaye haki ni mwenye haki, kama Kristo alivyo wa haki. 8 Kila atendaye dhambi ni wa shetani; kwa maana shetani ametenda dhambi tangu mwanzo. Mwana wa Mungu alikuja ili aziangamize kazi za shetani.
9 Mtu aliyezaliwa na Mungu haendelei na tabia ya kutenda dhambi, kwa maana ana asili ya Mungu; hawezi kuendelea kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.
Kutenda Haki Na Kupendana
10 Na hivi ndivyo tunavyoweza kutambua wazi kati ya walio watoto wa Mungu na walio watoto wa shetani. Mtu ye yote asiyet enda lililo haki si wa Mungu; wala asiyempenda ndugu yake si wa Mungu.
1 Petro 2:24 ESV
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi na kuishi kwa mambo ya uadilifu. Kwa majeraha yake mmeponywa.
Yohana 3:16-17 ESV
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Waebrania 10:26 ESV
Kwa maana tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
Mathayo 5:28 SW
Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
1 Wakorintho 6:9-10 ESV
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike: waasherati, waabudu sanamu, wazinzi, wapenzi wa jinsia moja, wezi, wachoyo, walevi, watukanaji, wanyang’anyi hawataurithi ufalme wa Mungu.
2 Wakorintho 5:21 ESV
Kwa ajili yetu alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye.
2 Wakorintho 5:17 ESV
Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya. Ya kale yamepita; tazama, mpya imekuja.
Warumi 5:12 ESV
Kwa hiyo, kama vile dhambi iliingia ulimwenguni kupitia mtu mmoja, na kifo kupitia dhambi; na hivyo kifo kikaenea kwa watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.
Isaya 64:6
Sisi sote tumekuwa kama mtu asiye safi, na matendo yetu yote ya haki ni kama vazi lililotiwa unajisi. Sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa kama upepo.