Mhariri Forum

Notifications
Clear all

Biblia inashauri nini kuhusu kukabiliana na majaribu?

Page 3 / 3
   RSS

0
Topic starter

What does the Bible advise on dealing with temptations?

40 Answers
0

1 Petro 5:8-11

Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo. Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo. Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara. Kwake yawe mamlaka milele! Amina.

0

Yakobo 1:2 ESV
Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mnapokutana na majaribu ya namna mbalimbali;

0

1 Petro 5:8-9

Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo. Muwe imara katika imani na kumpinga, mkijua kwamba ndugu zenu pote duniani wanapatwa na mateso hayohayo.

0

1 Wathesalonike 3:5

Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu ikapotea bure!

0

Yakobo 1:3 SW
Maana mnajua kwamba kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

0

Luka 11:4 SW
Na utusamehe dhambi zetu, kwa maana sisi wenyewe tunamsamehe kila mtu aliye na deni letu. Wala usitutie majaribuni.”

0

1 Yohana 2:16 ESV
Kwa maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na ulimwengu.

0

Waefeso 6:13 ESV
Kwa hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama imara.

0

Yakobo 1:14-15 ESV

Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya. Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo.

0

Mathayo 4:10
Kisha Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.

0

Zaburi 37:4
Jifurahishe katika Bwana, naye atakupa haja za moyo wako.

Page 3 / 3