Jinsi ya kujiunga WhatsApp

Posted by:

|

On:

|

,

WhatsApp ni nini?

WhatsApp ni programu isiyolipishwa na inayomilikiwa na Meta Platforms, kampuni ya teknolojia ya Marekani. WhatsApp inaruhusu watumiaji kutuma ujumbe wa SMS, ujumbe wa sauti na ujumbe wa video na pia kutuma picha.

Jinsi ya kujiunga whatsapp

Ili kutumia WhatsApp, jambo la kwanza utakalohitaji ni programu ya WhatsApp. Ikiwa hauna kwa simu, utahitaji kuipakua (kudownload) kutoka kwa Google Play Store. Ikiwa ni simu ya Android, lazima utumie Google Play Store; ikiwa ni iPhone, tumia App Store.

Mchakato ni sawa katika Google Play Store ama App Store. Tafuta “WhatsApp” na ubonyeze kitufe cha “search” bonyeza tokeo la kwanza, kisha ubonyeze “Install”. Kulingana na kasi ya mtandao wako, mchakato wa kudownload unaweza kudumu kutoka sekunde chache hadi dakika chache.

Sasa ukiwa na WhatsApp kwenye simu yako ya mkononi, ni wakati wa kuifungua. Kwa kuwa hii ni mara ya kwanza inafunguliwa, WhatsApp haina akaunti zozote na itakuuliza ujisajili kabla ya kuitumia kuwasiliana na watu.

Hatua za kujiunga na WhatsApp

Fungua programu ya WhatsApp. WhatsApp ina ikoni ya kisanduku cha kijani, changua lugha utakayoitumia.

Bonyeza kubali kisha uendelee (Accept and continue) na uendelee kukubali Sheria na Masharti (Terms and Conditions) ya WhatsApp.

Weka nambari yako ya simu. WhatsApp itatumia nambari hii kuthibitisha simu yako.

Gusa Inayofuata (Done) hapo chini ya skrini.

Gusa sawa (Yes) ili kuthibitisha nambari ya simu uliyoweka (Verify phone number).

Ruhusu WhatsAPP ithibitishe namba kwa kubonyeza Endelea. (Continue)

Subiri hadi upokee ujumbe otomatiki kutoka kwa WhatsApp. Utapokea SMS iliyo na nambari ya kuthibitisha yenye tarakimu sita (Verification code).

Usipoipokea, bofya kitufe cha “Receive a call”. Utapigiwa simu na WhatsApp wakwambie hizo tarakimu sita (Verification code), andika hiyo namba chini kwa sababu utaitumia baadaye.

Weka hiyo nambari wamekutumia kwenye WhatsApp (hapo kwa verification box). Kisha nambari yako ya simu itathibitishwa.

Maelezo ya jalada: gusa kitufe cha kuweka picha (profile photo): Mduara wenye uko na kamera. Gusa kitufe hiki ili kupiga picha mpya au uchague picha kutoka kwa safu ya kamera yako.

Bofya  andika jina lako hapa (Enter your username) na uweke jina lako: hii ni jina lako . Hili ndilo jina ambalo marafiki zako wataona watakapokutumia ujumbe, kisha gusa Inayofuata.

Sasa, uko tayari kutumia WhatsApp.

Ujumbe wako wa kwanza wa WhatsApp

Tayari una kila kitu tayari. Kwa kuwa WhatsApp yako ni mpya kabisa, unaanza mtupu na bila mazungumzo yoyote. Ili kufungua gumzo lako la kwanza, bonyeza kitufe cha ujumbe na orodha ya watu ambazo umehifadhi kwenye simu yako ambao wako na WhatsApp zitaletwa . Huenda ukahitaji kwanza kutoa ruhusa kwa WhatsApp kwenye simu yako ili kupata “contacts” zako.

Gusa mtu unayetaka kuzungumza naye, na sasa unaweza kutuma ujumbe wako wa kwanza wa WhatsApp. Andika maandishi kwenye kisanduku hapo chini na ubonyeze kitufe cha mshale ili kuituma. Mbali na kutuma ujumbe, unaweza kupiga simu, simu za video, na picha.