Jinsi ya kupika tambi

Posted by:

|

On:

|

,

Tambi ndio pasta au spaghetti kwa kiingereza. Hujui jinsi ya kupika tambi? Usijali, uko katika sehemu sahihi ya kupata maagizo ya kupika tabi.

Viungo (Ingredients)

  • Tambi 450-900g (Spaghetti)
  • Maji
  • Vijiko 1-2 vya chumvi

Inatosha watu 4-8

Maagizo ya kupika tambi

  1. Jaza sufuria kubwa na maji: Ikiwa unapanga kupika karibu 700-900g ya tambi, tumia sufuria yenye uwezo wa lita 5-6, jaza karibu robo tatu ya maji.
  2. Ongeza chumvi na uchemsha: Mimina kijiko moja au viwili vya chumvi ndani ya maji na kisha weka kifuniko kwenye sufuria na uwache maji yachemke kwa nguvu.
  3. Weka tambi kwenye sufuria: Weka tambi kwa sufuria kisha ukoroge na kijiko. Baada ya sekunde chache maji yanapaswa kuanza kuchemka tena. Unaenza vunja tambi ikiwa unapendelea kula tambi fupi.
  4. Soma maagizo kwenye kifurushi ili ujue ni dakika ngapi za kupika tambi unahitaji. Kumbuka kuchanganya mara kwa mara ili kuzuia tambi kushikamana pamoja. Usifunike sufuria wakati wa kupika tambi.
  5. Onja tambi ili kuona ikiwa zimeiva. Ikiwa unapouma kwenye tambi unahisi kuwa bado ni ngumu katikati, ongeza dakika 1 au 2 ya kupika na kisha jaribu nyingine.
  6. Tambi zikiwa tayari mwaga maji yaliyozalia na upakue na mchuzi uupendao.

Tambi na mchuzi wa nyanya uliojitengenezea

Viungo (Ingredients)

  • Tambi 700 g, kupikwa na kumwaga maji (Fuata maagizo hapo juu)
  • Nyanya 4-8 kubwa
  • Vijiko 2 vya mafuta ya mzeituni (olive oil)
  • Kitunguu nyekundu, kilichokatwa
  • Kitunguu saumu (3 cloves)
  • Dania
  • Pilipili
  • Chumvi

Inatosha watu 2-3

  1. Kutengeneza mchuzi wa nyanya: Unaenza tumia blender ya umeme kutengeneza mchuzi, kama unatumia blender hakikisha umetoa maganda ya nyanya
  2. Ama unaweza kukata nyanya zilizopigwa kwa mkono na kisu au unaweza kuziponda tu kwa nyuma ya kijiko baada ya kuzipika kwenye moto mdogo.
  3. Kaanga vitunguu mpaka vigeuke rangi: Pasha vijiko viwili vya mafuta ya mzeituni kwenye sufuria. Wakati mafuta yamechemka, ongeza vitunguu vyekundu vilivyokatwa. Koroga vitunguu mara kwa mara vinapoiva ili visishikane na sufuria.
  4. Pia ongeza vitunguu saumu na pilipili: Chambua na ukate kitunguu saumu na pilipili hoho ama pilipili yoyote upendaye. Kaanga viungo hivyo kwa takriban sekunde 30 kabla ya kuendelea.
  5. Mimina mchuzi wa nyanya uliotengeneza kwenye sufuria na uongeze chumvi: Changanya viungo vyote na uache viive, onja mchuzi wako unapoiva ili kuona ikiwa unahitaji kuongeza chumvi au pilipili zaidi.
  6. Acha mchuzi upike juu ya moto wa kati kwa dakika 30. Usiweke kifuniko kwenye sufuria kwani hii itafanya mchuzi kupungua na kuwa mzito kidogo. Koroga mara kwa mara ili kuzuia mchuzi kushika chini ya sufuria.
  7. Kata majani ya dania na uongeze kwenye mchuzi. Onja mchuzi tena ili kuona ikiwa ni bora kuongeza chumvi au pilipili zaidi.
  8. Mimina mchuzi wa nyanya juu ya tambi na kijiko na ukule chakula chako.

.