,

Jinsi rahisi sana ya kupika keki na jiko

Unaweza kupika keki katika jiko lako. Ni rahisi sana, kile unachotakiwa kufanya ni kuchanganya unga wa ngano unaoupenda na vanila na chokoleti. Kisha washa makaa kwenye jiko lako na weka sufuria juu ya makaa ili sufuria ipate moto kidogo. Kisha weka unga ulioukanda kwenye sufuria na ufunike. Eneza makaa ya moto juu ya ufuniko na kando ya sufuria na ongoja hadi keki kupikwa kabisa.

Jinsi ya kupika keki

Viungo/ Ingredients

Keki ya Mdalasini ya Ngano / Cinnamon Cake

  • Vikombe 3 (360 g) vya unga wa ngano
  • Vijiko 2 (15.5 g) vya mdalasini (cinnamon)
  • Mayai 3
  • Kikombe ½ (100 g) cha sukari kahawia (brown sugar)
  • Kikombe ½ (100 g) cha majarini (margarine)
  • Kijiko 1 (12 g) cha poda ya kuoka (baking powder)
  • Kijiko 1 cha chumvi

Hutengeneza keki 1

Keki ya Marumaru/ Marble Cake

  • Kikombe ½ (100 g) cha majarini (margarine)
  • Kikombe 1 (200 g) cha sukari
  • 3 mayai
  • Kikombe 1 (125 g) cha unga wa ngano (all-purpose flour)
  • Kijiko 1 (4 g) cha poda ya kuoka (baking powder)
  • Kijiko 1 cha chumvi
  • Vijiko 2 (30 ml) vya vanilla
  • Vijiko 2 (30 ml) vya maziwa
  • Vijiko 2 (14 g) vya poda ya kakao (cocoa powder)

Hutengeneza keki 1

Jinsi ya kupika Keki ya Mdalasini ya Ngano

  1. Changanya unga, mdalasini, hamira, na chumvi: Tafuta bakuli kubwa na uweke vikombe 3 (360 g) vya unga wa ngano ndani yake. Koroga vijiko 2 (15.5 g) vya mdalasini, kijiko 1 (14.8 ml) (12 g) cha poda ya kuoka, na chumvi kidogo. Weka hivo viungo vya kavu kando.
  2. Changanya majarini na sukari ya kahawia kwa dakika 3 hadi 5: Weka kikombe cha 1/2 (100 g) ya majarini kwenye bakuli tofauti na kuongeza 1/2 kikombe (100 g) cha sukari ya kahawia (brown sugar). Tumia kijiko kuchanganya majarini na sukari ya kahawia hadi iwe nyepesi na laini.
  3. Vunja yai moja kwenye mchanganyiko wa majarini na sukari ya kahawia: Kisha changanya hadi iwe imeunganishwa. Ongeza mayai mbili iliyobaki, moja kwa wakati.
  4. Koroga viungo vya kwanza kwenye mchanganyiko ambao umetegeneza: Polepole changanya hivo viungo mbili na ukande unga hadi iwe laini kabisa. Hakikisha unachanganya pande zote za bakuli.
  5. Washa makaa kwenye jiko: Jaza sehemu ya juu ya jiko na makaa na ufungue mlango wa jiko ili hewa iingie. Weka baadhi ya makaa uliyotumika awali kwenye chemba iliyo chini. Washa makaa na kisha upepete ili makaa yashike moto.
  6. Paka sufuria mafuta na ueneze unga ndani yake: Paka pande zote za sufuria na majarini (mafuta ya kupika) ili kuzuia keki kushikana na sufuria. Mimina unga ambao umekanda kwenye sufuria iliyotiwa mafuta.
  7. Funika sufuria na ujaze na makaa ya moto: Weka funiko kwenye sufuria na uweke vipande 3 hadi 5 vya makaa ya moto juu yake.  Ukiweka makaa juu ya kifuniko unahakikisha joto linasambazwe kwenye keki nzima.
  8. Weka sufuria kwenye jiko na uoka keki kwa dakika 30: Kwa uangalifu sana inua sufuria ya moto na kuiweka juu ya makaa ya moto ya jiko. Oka keki hadi iive kabisa. Ili kupima ikiwa keki imeiva, ingiza kijiko katikati ya keki, ikiwa kimetoka kikavu kabisa, basi keki imeiva.
  9. Toa sufuria kwenye jiko na upoze keki kwenye sufuria: Keki inapomaliza kuoka, inua sufuria kwa uangalifu kutoka kwenye jiko na kuiweka kando. Ondoa kifuniko na makaa kutoka juu ya sufuria, lakini acha keki ndani ya sufuria. Acha keki ipoe kabisa kabla ya kuiondoa kwenye sufuria. Ikiwa utajaribu kuondoa keki wakati bado ni moto, haitashikana.
  10. Pakua keki yako: Ukitaka unaenza changanya juu ya keki whipped cream ama chocolate frosting. Kata na ukule keki yako.

Ikiwa unataka kuhifadhi keki iliyobakia, weka keki kwenye chombo kisichopitisha hewa na pahali penye joto la kawaida kwa hadi siku mbili.

Jinsi ya Kupika Keki ya Marumaru/ Marble Cake

  1. Changanya majarini na sukari kwa dakika 1 hadi 2: Weka kikombe nusu 1/2 (100 g) ya majarini kwenye bakuli kubwa ya kuchanganya na kuongeza kikombe 1 (200 g) cha sukari. Tumia kijiko kuchanganya majarini na sukari kwa kasi ya wastani hadi iwe nyepesi na laini.
  2. Vunja yai moja kwenye mchanganyiko wa majarini na sukari: Kisha changanya hadi iwe imeunganishwa. Ongeza mayai mbili iliyobaki, moja kwa wakati.
  3. Ongenza unga, poda ya kuoka na chumvi kisha ukoroge: Ongeza kikombe 1 (125 g) cha unga wa ngano, kijiko 1 (g 4) cha poda ya kuoka, na chumvi kidogo. Koroga mpaka iwe laini.
  4. Changanya vanilla na maziwa. Mimina vijiko 2 (30 ml) vya vanila na vijiko 2 (30 ml) vya maziwa kwenye bakuli na tumia kijiko ili kuvikoroga. Ikiwa unga ni mzito sana wa kukoroga kwa urahisi, ongeza maziwa na vanila ili kuulegeza. Ukimaliza kukoroga umetegeneza unga wa vanila Ikiwa ungependa tu kutengeneza keki ya vanila, unaweza acha kutumia chokoleti (cocoa powder).
  5. Koroga na kakao (cocoa): Ili kutengeneza keki ya marumaru au pundamilia, weka kikombe 1 (240 ml) cha mchanganyiko wa unga wa vanila kwenye bakuli tofauti na uweke kando. Kisha koroga vijiko 2 (14 g) vya cocoa powder kwenye unga wa mchanganyiko uliosalia (kwenye bakuli lako la asili). Ukimaliza kukoroga umetengeneza mchanganyiko wa unga wa chokoleti.
  6. Paka sufuria mafuta na ueneze unga ndani yake: Paka pande zote za sufuria na majarini (mafuta ya kupika) ili kuzuia keki kushikana na sufuria.
  7. Changanya unga wa vanila na unga wa chokoleti (in step 5) kwenye sufuria ili kutengeneza marumaru. Ukitumia bakuli ndogo ama kikombe, chovya bakuli kwenye mchanganyiko wa unga wa chokoleti na kumwaga kwenye sufuria iliyotiwa mafuta. Chukua bakuli ndogo ingine na uchovye kwa unga wa vanilla (uliouweka kando), kisha umwage pia kwenye sufuria. Endelea kufanya hivyo hadi mchanganyo wa unga uishe -Bakuli moja ya unga wa chokoleti na kisha bakuli ingine ya unga wa vanila, ukimwaga kwa sufria.
  8. Washa makaa kwenye jiko: Jaza sehemu ya juu ya jiko na makaa na ufungue mlango wa jiko ili hewa iingie. Weka baadhi ya mkaa uliotumika awali kwenye chemba iliyo chini. Washa makaa na kisha upepete ili makaa yashike moto.
  9. Pasha sufuria kubwa kwa dakika 5 hadi 10: Tafuta sufuria kubwa kuliko ya iliyo na keki, kisha iweke juu ya jiko. Weka mawe 3 kwenye hiyo sufuria au mimina sentimita mbili na nusu ya mchanga ndani yake. Funika hiyo sufuria na uiruhusu iwe moto kwa dakika 5 hadi 10.
  10. Weka sufuria ya keki kwenye sufuria kubwa na uifunike kwa kifuniko na mkaa: Weka sufuria iliyojaa unga wa keki ndani ya sufuria kubwa ya mchanga au mawe. Weka kifuniko kwenye sufuria kubwa na uweke kwa uangalifu makaa ya moto juu ya kifuniko.
  11. Oka keki iliyofunikwa kwa dakika 50 hadi 60: Ikiwa makaa yanaonekana kuisha kabla ya keki kumalizika, ongeza makaa zaidi katikati ya muda wa kuoka. Oka keki hadi iive kabisa. Ili kupima ikiwa keki imeiva, ingiza kijiko katikati ya keki, ikiwa kimetoka kikavu kabisa, basi keki imeiva.
  12. Toa sufuria kwa jiko na upoze keki kwenye sufuria. Inua sufuria kwa uangalifu kutoka kwenye jiko na uiweke kando. Inua kifuniko na makaa kutoka juu ya sufuria, lakini acha keki ndani ya sufuria ipoe kabisa kabla ya kuitoa.
  13. Pakua keki yako: Ukitaka unaenza changanya juu ya keki whipped cream ama chocolate frosting. Kata na ukule keki yako.

Ikiwa unataka kuhifadhi keki iliyobakia, weka keki kwenye chombo kisichopitisha hewa na pahali penye joto la kawaida kwa hadi siku mbili.

4 responses to “Jinsi rahisi sana ya kupika keki na jiko”

Related Posts