Kinyume cha kusanya

Posted by:

|

On:

|

Kusanya ni leta au weka pamoja watu au vitu vingi.

Mfano: Mama anakusanya kuni.

Kinyume cha kusanya

Kinyume cha kusanya ni tawanya au sambaza.

Tawanya ni eneza kitu kila mahali au sehemu.

Mfano: Mtoto anatawanya karatasi kila mahali.

Sambaza ni eneza habari au kitu ili kiwafikie watu wengi.

Mfano: Maadui zangu wamesambaza uvumi kuniharibia jina.