Kinyume cha neno choma

Posted by:

|

On:

|

Choma ni :

Penyeza kitu chenye ncha

Mfano: Salimu alijichoma kidole kwa sindano.

Teketeza kwa moto

Mfano: Mwalimu alituagiza kuyachoma majani yote baada ya kuyafyeka.

Sababisha joto kali mwilini

Mfano: Jua lilimchoma Janet mpaka ngozi yake ikabambuka.

Kinyume cha choma

Kinyume cha choma kinategemea maana unayojusudia:

Kinyume cha choma (penyeza kitu chenye ncha) ni chomoa au toa.

Chomoa ni toa kwa kuvuta nje kitu ambacho kimo ndani ya kitu kingine.

Toa ni ondoa kitu kilicho ndani na kukiweka nje.

Mfano: Saumu alichomoa kisu kutoka katika ala akamchinja kuku.

Kinyume cha choma (teketeza kwa moto) ni zima.

Zima ni fanya kitu kisiendelee kuwaka.

Kinyume cha choma (sababisha joto mwilini) ni poza.

Poza ni fanya kitu kiwe baridi, fanya ipoe.