Mfalme ni mtawala wa kiume mwenye mamlaka kamili ya kutawala milki bila ya mbinu zake kudadisiwa na raia bali mamlaka hayo huyarihi kutoka kwa mzazi wake wa kiume ambaye naye alikuwa mfalme.
Kinyume cha mfalme
Kinyume cha mfalme ni: malkia, raia, mtumishi nk.
Malkia ni mke wa mfalme; mtawala wa kike mwenye mamlaka ya kutawala miliki atokaye katika ukoo wa kifalme.
Raia ni mtu wa kawaida tu katika muktadha wa uongozi wa nchi; mtawaliwa.
Mtumishi ni mtu afanyaye kazi ya kulipwa mshahara, kutokana na kazi anayoifanyia umma; anayeifanyia serikali kazi na kulipwa mshahara.
Kinyume cha malkia
Kufuatia ufafanuzi wa hapo juu, Kinyume cha malkia ni; mfalme, raia au mtumishi.