Kinyume cha neno zama

Posted by:

|

On:

|

Zama ni:

Ingia chini ya maji kwa mfano ya bahari, mto, bwawa au ziwa.

Mfano: Mtalii alizama majini na kufa alipokuwa anaogelea.

Kwenda chini kwa jua au mwezi na kupotea machoni

Mfano: Kila siku jua linapokuchwa jioni, huzama upande wa magharibi.

Kinyume cha zama

Kinyume cha zama ni elea.

Elea ni kuwa juu ya uowevu wowote au maji bila kuzama.

Mfano: Karatasi inaelea juu ya maji.