Rafiki ni mwanamume au mwanamke anayeaminiana na mwingine na anayeshirikiana naye katika mambo mengi
Visawe vya rafiki ni:
- mwandani
 - sahibu
 
Wingi wa rafiki
Wingi wa rafiki ni marafiki.
Umoja wa marafiki
Umoja wa marafiki ni rafiki.
Mifano ya umoja na wingi wa rafiki katika sentensi
| Umoja | Wingi | 
| Huyu ni rafiki yangu ambaye tulienda shule ya upili pamoja. | Hawa ni marafiki zangu ambao tulienda shule ya upili pamoja. | 
| Wewe ni rafiki wake? | Nyinyi ni marafiki wao? | 
| Wewe ndiye mtu pekee ulimwenguni ambaye ninaweza kumwita rafiki yangu. | Ninyi ndio watu pekee ulimwenguni ambao ninaweza kuwaita marafiki zangu. | 
| Rafiki yako mpendwa. | Marafiki wenu wapendwa. | 
| Una rafiki mzuri sana. | Mna marafiki wazuri sana. | 
| Wewe au rafiki yako sio sahihi. | Nyinyi au marafiki wenu sio sahihi. | 
| Nilimuona rafiki yangu akitembea kwa mbali. | Tuliwaona marafiki zetu wakitembea kwa mbali. | 
| Nilikutana na rafiki yangu wakati nikitembea huko. | Tulikutana na marafiki zetu wakati tukitembea huko. | 
| Nilikutana na rafiki yangu wa zamani karibu na benki. | Tulikutana na marafiki zetu wa zamani karibu na benki. | 
| Pea rafiki yako pesa. | Pea marafiki zenu pesa. | 
| Rafiki yangu aliingia nyumbani kwangu. | Marafiki wetu waliingia nyumbani kwetu. | 
| Wewe ni rafiki yangu bora. | Nyinyi ni marafiki zetu bora. | 
| Alikutana na rafiki yake wakati alienda kutembea. | Walikutana na marafiki zao wakati walienda kutembea. | 
| Nikiwa njiani kurudi nyumbani, nilikutana na rafiki yangu. | Tukiwa njiani kurudi nyumbani, tulikutana na marafiki zetu. | 
| Nilimpigia simu rafiki yangu. | Tuliwapigia simu marafiki zetu. | 
| Nilikutana na rafiki yangu wa zamani. | Tulikutana na marafiki zetu wa zamani. | 
| Ningependa kuwa na rafiki wa kuwasiliana naye. | Tungependa kuwa na marafiki wa kuwasiliana nao. | 
| Nina rafiki ambaye baba yake ni mpiga kinanda maarufu. | Tuna marafiki ambao baba zao ni wapiga kinanda maarufu. | 
| Nilipata barua kutoka kwa rafiki yangu huko Marekani. | Tulipata barua kutoka kwa marafiki zetu huko Marekani. | 
| Nilikutana na rafiki yako. | Tulikutana na marafiki zenu. | 
| Alimpigia simu rafiki yake jana jioni. | Waliwapigia simu marafiki zao jana jioni. | 
| Rafiki yangu anapenda mbwa sana. | Marafiki zetu wanapenda mbwa sana. | 
| Nitakaa na rafiki yangu kwa muda. | Tutakaa kwa marafiki zetu kwa muda. |