Ufunguo ni:
- Kifaa cha kufungia na kufungulia kufuli, mlango, sanduku na kadhalika.
- Kifaa kideogo kwenye saa cha kuijaza kamani ili saa iende na pia kurekebishia mwezi, siku na tarehe
- Vielelezo au alama zilizotumika katika ramani au mchoro.
Wingi wa ufunguo
Wingi wa ufunguo ni funguo.
Umoja wa funguo
Umoja wa funguo ni ufunguo.
Mifano ya umoja na wingi wa ufunguo katika sentensi
Umoja | Wingi |
Hawezi kuwa amepoteza ufunguo wake. | Hawawezikuwa wamepoteza funguo zao. |
Umepata wapi ufunguo? | Mmepata wapi funguo? |
Ufunguo wangu uko wapi? | Funguo zetu ziko wapi? |
Umepata ufunguo wako? | Mmepata funguo zenu? |
Alibahatika kupata ufunguo wake. | Walibahatika kupata funguo zao. |
Baba yangu hupoteza ufunguo wake angalau mara moja kwa wiki. | Baba zetu hupoteza funguo zao angalau mara moja kwa wiki. |
Ufunguo huu sio wangu. | Funguo hizi sio zangu. |
Unahitaji ufunguo? | Mnahitaji funguo? |
Natafuta ufunguo wangu. | Tunatafuta funguo zetu. |
Niliacha ufunguo wangu mezani. Unaweza kuniletea? | Tuliacha funguo zetu mezani. Mnaweza kutuletea? |
Akachungulia chumbani kutafuta ufunguo wake. | Wakachungulia chumbani kutafuta funguo zao. |
Hajui ni wapi aliacha ufunguo wake. | Hawajui ni wapi waliacha funguo zao. |
Amepoteza ufunguo wake. | Wamepoteza funguo zao. |
Alipata ufunguo aliuodhani ameupoteza. | Walipata funguo walizodhani wamezipoteza. |
Je, unajua ambapo aliweka ufunguo? | Je, mnajua ambapo waliweka funguo? |
Akamkabidhi ufunguo. | Waliwakabidhi funguo. |
Sikutaka kutumia muda zaidi kutafuta ufunguo wangu. | Hatukutaka kutumia muda zaidi kutafuta funguo zetu. |
Akaacha ufunguo wake mezani. | Wakaacha funguo zao mezani. |
Hakumbuki ni wapi aliweka ufunguo wake. | Hawakumbuki ni wapi waliweka funguo zao. |
Inawezekana kwamba nilisahau ufunguo wangu. | Inawezekana kwamba tulisahau funguo zetu. |
Nimepoteza ufunguo wangu. | Tumepoteza funguo zetu. |
Akafungia ufunguo wake kwenye gari lake. | Walifungia funguo zao kwenye magari yao. |
Ulipataje ufunguo? | Mlipataje funguo? |
Chukua ufunguo kwa kaka yako. | Chukua funguo kwa kaka zako. |
Umesahau funguo zako. | Umesahau funguo zako. |
Ufunguo wako uko wapi? | Funguo zako ziko wapi? |
Nipe ufunguo ili niweze kufungua mlango. | Tupe funguo ili tuweze kufungua milango. |
Lete ufunguo kwa ndugu yako. | Lete funguo kwa ndugu zako. |
Nimefanya nini na ufunguo wangu? | Tumefanya nini na funguo zetu? |
Unajua ufunguo aliweka wapi? | Unajua funguo waliweka wapi? |
Ufunguo huu si wangu. | Funguo hizo si zetu. |
Hukuona ufunguo wangu? | Hukuona funguo zetu? |
Nikadondosha ufunguo wangu. | Tukadondosha funguo zetu. |
Nimefungia ufunguo wangu kwenye gari langu. | Tumefungia funguo zetu kwenye magari yetu. |
Chukua ufunguo wa gari lake. | Chukua funguo za magari yao. |
Anatafuta ufunguo zake. | Wanatafuta funguo zao. |
Hii ni mara ya kwanza nimepoteza funguo zangu. | Hii ni mara ya kwanza tumepoteza funguo zetu. |
Ulimpa nani ufunguo wa nyumba? | Mliwapa nani funguo za nyumba? |
Mwambie kuwa natafuta ufunguo. | Waambie kwamba tunatafuta funguo. |