Wingi wa kivumishi changu

Changu ni kivumishi kimilikishi katika nafsi ya kwanza umoja.

Wingi wa changu

Wingi wa changu ni vyetu.

Vyangu ni kivumishi-kimilikishi cha ngeli ya [ki-/vi-] cha nafsi ya kwanza umoja kuonyesha vitu fulani vinamilikiwa na mimi. Kwa hivyo haezi kuwa wingi wa changu.

Vyetu ni kivumishi-kimilikishi cha ngeli ya [ki-/vi-] cha nafsi ya kwanza wingi cha kuonyesha vitu fulani vinamilikiwa na sisi. Kwa hivyo, vyetu ndio neno kamili la wingi wa changu.

Mifano katika sentensi

  • Kitabu hiki ni changu. (Vitabu hivi ni vyetu.)
  • Kiti changu kimevunjika. (Viti vyetu vimevunjika.(
  • Kikapu changu kimejaa matunda. (Vikapu vyetu vimejaa matunda.)
Related Posts