Changu ni kivumishi kimilikishi katika nafsi ya kwanza umoja.
Wingi wa changu
Wingi wa changu ni vyetu.
Vyangu ni kivumishi-kimilikishi cha ngeli ya [ki-/vi-] cha nafsi ya kwanza umoja kuonyesha vitu fulani vinamilikiwa na mimi. Kwa hivyo haezi kuwa wingi wa changu.
Vyetu ni kivumishi-kimilikishi cha ngeli ya [ki-/vi-] cha nafsi ya kwanza wingi cha kuonyesha vitu fulani vinamilikiwa na sisi. Kwa hivyo, vyetu ndio neno kamili la wingi wa changu.
Mifano katika sentensi
- Kitabu hiki ni changu. (Vitabu hivi ni vyetu.)
- Kiti changu kimevunjika. (Viti vyetu vimevunjika.(
- Kikapu changu kimejaa matunda. (Vikapu vyetu vimejaa matunda.)