Mistari ya biblia kuhusu mahusiano

Posted by:

|

On:

|

Mistari hiii inatoa mwongozo na hekima kuhusu mambo mbalimbali ya mahusiano kama vile: upendo, uaminifu, urafiki, na ndoa, kama inavyoonyeshwa katika Biblia.

Mistari ya biblia kuhusu mahusiano

Marko 10:9 BHN

Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe.”

1 Petro 4:8 SRUV

Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.

Waefeso 4:2-3 BHN

Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni nyinyi kwa nyinyi kwa mapendo. Fanyeni bidii ya kuhifadhi umoja uletwao na Roho kwa kuzingatia amani iliyo kati yenu.

Mhubiri 4:9-10 BHN (BHN: Biblia Habari Njema)

Ni afadhali kuwa wawili kuliko mtu kuwa peke yake. Kwa sababu wawili watapata tuzo la kazi yao. Ikijatokea mmoja akaanguka, huyo mwenzake atamwinua. Lakini ole wake aliye peke yake akianguka! Huyo hatakuwa na mtu wa kumwinua!

1 Wakorintho 13:4 NEN (NEN: Neno: Bibilia Takatifu)

Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi.

Mithali 17:17 SRUV (SRUV: Swahili Revised Union Version)

Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.

1 Wakorintho 15:33 SRUVDC (SRUVDC: Swahili Revised Union Version)

Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

Yohana 3:18 NEN

Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

Mithali 13:20 SRUV

Nenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.

1 Wathesalonike 5:11 BHN

Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa.

2 Wakorintho 6:14 BHN

Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?

Mithali 27:17 SRUV

Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.

Mithali 15:1 SRUV

Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.

Warumi 12:9 NEN

Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema.

Wakolosai 3:14 – Bibilia Takatifu

Juu ya haya yote, vaeni upendo ambao unaunganisha mambo haya kuwa kitu kimoja kilicho kikamilifu.

Mithali 18:22 NMM (NMM: Neno: Maandiko Matakatifu)

Apataye mke apata kitu chema naye ajipatia kibali kwa BWANA.

Wakolosai 3:18-19 BHN

Enyi wake, watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana. Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.

Mithali 10:12 NEN

Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote.

Mithali 4:23 SRUVDC

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Wafilipi 2:4 SRUV

Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Mithali 31:11 SRUV

Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.

Mathayo 19:6 BHN

Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asikitenganishe.”

Mithali 18:24 SRUV

Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

Mithali 31:10-31 SRUV

Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu. Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku. Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia. Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.

Mithali 19:14 RSUVDC (RSUVDC: Biblia Kiswahili)

Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.

Mithali 3:3 SRUV

Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

1 Timotheo 5:1 (NIV)

“Usimkemee mtu mzee kwa ukali, bali msihi kama baba yako. Watendee vijana kama ndugu.”

Waefeso 4:3 Bibilia Takatifu

Muwe wepesi wa kutaka kudumisha umoja wa Roho kwa sababu ya amani inayowafunga pamoja.

Mithali 12:4 NEN

Mke mwenye tabia nzuri ni taji ya mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.

1 Wakorintho 13:4-5 BHN

Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya