Mistari ya biblia kuhusu upendo

Posted by:

|

On:

|

Upendo ndio nguvu kubwa zaidi ulimwenguni. Ni kiungo kinachtunganisha sisi kwa sisi na kwa Mungu. Upendo wa kweli ni kumpenda mwenzako na mungu wako. Hizi ni mistari ya biblia kuhusu upendo.

Mistari ya biblia kuhusu upendo

1 Wakorintho 13:4-8 BHN

Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote. Upendo hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita.

1 Wakorintho 13:13 BHN

Sasa yanadumu haya matatu: Imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.

1 Petro 4:8 SRUV

Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.

Mithali 3:3 SRUV

Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

Yohana 13:34 SRUV

Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

1 Yohana 4:7-8 SRUV

Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.

Mithali 17:17 NEN

Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.

Warumi 13:10 NEN

Upendo haumfanyii jirani jambo baya. Kwa hiyo upendo ndio utimilifu wa sheria.

Mithali 10:12 NEN

Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote.

Yohana 15:12 NEN

Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi.

1 Yohana 4:18 SRUV

Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.

Waefeso 4:2 BHN

Muwe daima wanyenyekevu, wapole na wenye saburi; vumilianeni nyinyi kwa nyinyi kwa mapendo.

Wakolosai 3:14 BHN

Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.

Waefeso 5:25 BHND

Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake.

1 Wakorintho 16:14 SRUV

Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.

1 Yohana 4:8 NEN

Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo.

1 Petro 4:8 BHND

Zaidi ya yote pendaneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi.

Wimbo Ulio Bora 8:7 BHN

Maji mengi hayawezi kamwe kulizima, mafuriko hayawezi kulizamisha. Mtu akijaribu kununua pendo, akalitolea mali yake yote, atakachopata ni dharau tupu.

Warumi 12:9 NEN

Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema.

Wakolosai 3:14 BHN

Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.

Waefeso 5:2 BHN

Upendo uongoze maisha yenu kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama tambiko yenye harufu nzuri na sadaka impendezayo Mungu.

Warumi 5:8 SRUV

Bali Mungu aonesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

1 Yohana 4:11 SRUV

Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.

1 Wakorintho 16:14 SRUV

Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.

1 Yohana 4:18-20 – Bibilia Takatifu

18 Katika upendo hakuna woga; upendo ulioka milika hufukuza woga wote, kwa sababu woga hutokana na adhabu. Mtu mwenye woga hajakamilishwa katika upendo. 19 Tunapenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20 Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” na huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona.