Mistari ya biblia ya ulinzi na usalama

Posted by:

|

On:

|

Ulinzi na usalama wetu unatoka kwa Mungu, tunahisi salama kweli tunapoweka maisha yetu mikononi mwa Bwana. Yeye ni mkuu kuliko woga wetu wote. Ana uwezo wa kutulinda dhidi ya adui na kutupa ushindi katika pambano yetu, hata wakati ambapo hakuna mtu anayetuamini. Hapa tutakupa mistari ya biblia ya ulinzi na usalama yeye itatupa hakikisho kuwa Mungu ako nazi katika kila jambo tufanyalo.

Mistari ya biblia ya ulinzi na usalama

Zaburi 4:8 SRUVDC

Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, BWANA, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

Mithali 18:10 SRUV

Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.

Zaburi 91:1-2 BHN

Anayekaa chini ya ulinzi wa Mungu Mkuu, anayeishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu, ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu: “Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu; Mungu wangu, ninayekutumainia!”

Isaya 41:10 BHN

Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe. Usifadhaike, mimi ni Mungu wako. Nitakuimarisha na kukusaidia; nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.

Mithali 3:24 NEN

Ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.

Zaburi 121:3 BHN

Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii.

Zaburi 16:8 BHN

Namweka Mwenyezi-Mungu mbele yangu daima; yuko pamoja nami, wala sitatikisika.

Isaya 26:3 SRUV

Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

Zaburi 32:7 BHN

Wewe ndiwe kinga yangu; wewe wanilinda katika taabu. Umenijalia shangwe za kukombolewa.

Mithali 29:25 SRUV

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.

Zaburi 23:4 BHN

Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda.

Zaburi 27:1 BHN

Mwenyezi-Mungu ni mwanga wangu na wokovu wangu, ni nani nitakayemwogopa? Mwenyezi-Mungu ni ngome ya maisha yangu, sitamwogopa mtu yeyote.

Zaburi 56:3-4 BHN

Ee Mungu Mkuu, hofu inaponishika, mimi nakutumainia wewe. Namtumainia Mungu na kusifu neno lake; namtumainia Mungu, wala siogopi. Binadamu dhaifu atanifanya nini?

Warumi 8:38-39 SRUV

Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Waebrania 13:6 BHN

Ndiyo maana tunathubutu kusema: “Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?”

Zaburi 91:4 BHN

Atakufunika kwa mabawa yake, utapata usalama kwake; mkono wake utakulinda na kukukinga.

Mithali 2:7 SRUV

Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu.

Zaburi 37:28 BHN

Maana Mwenyezi-Mungu hupenda uadilifu, wala hawaachi waaminifu wake. Huwalinda hao milele; lakini wazawa wa waovu wataangamizwa.

Zaburi 112:7 BHN

Hana haja ya kuogopa akipata habari mbaya; ana moyo thabiti na humtegemea Mwenyezi-Mungu.

Isaya 54:17 RSUVDC

Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.

Nahumu 1:7 SRUV

BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.

Zaburi 62:2 SRUV

Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika.

Zaburi 18:2 BHN

Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu.

Zaburi 46:1-2 BHN

Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu; yeye ni msaada wetu daima wakati wa taabu. Kwa hiyo hatutaogopa chochote, dunia ijapoyeyuka na milima kutikisika kutoka baharini.

Zaburi 118:6 SRUVDC

BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

Zaburi 23:1-4 BHN

Mwenyezi-Mungu ni mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Hunipumzisha kwenye malisho mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu, na kuirudishia nafsi yangu nguvu mpya. Huniongoza katika njia sawa kwa hisani yake. Nijapopita katika bonde la giza kuu la kifo, sitaogopa hatari yoyote, maana wewe ee Mwenyezi-Mungu u pamoja nami; gongo lako na fimbo yako vyanilinda.

Yohane 10:28-29 BHN

Mimi nawapa uhai wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu. Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wala hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba.

Zaburi 125:2 BHN

Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima, ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo watu wake, tangu sasa na hata milele.