Category: Maana ya maneno
Maana ya neno abee! na English translation
Maana ya neno abee! (Kihisishi) neno la kuitikia wito litumiwalo na wanawake wanapoitwa. Visawe ni: bee, beka. Abee! Katika Kiingereza (English translation) Abee! Katika Kiingereza ni: Yes. Read more
Maana ya neno abedari na English translation
Maana ya neno abedari 1. (Nomino katika ngeli ya [i-/zi-]) (bah) roda inayotumiwa kuvutia vitu kwenye jahazi. Kisawe ni kapi. 2. (Kielezi) neno la kumtahadharisha mtu. Visawe ni: simile!, kaa chonjo! Abedari Katika Kiingereza (English translation) Abedari katika Kiingereza hutegemea maana unayokusudia: Abedari inayovuta vitu kwenye jahazi ni: Pulley. Abedari ya kumtahadharisha mtu ni: Careful,… Read more
Maana ya neno abdi na English Translation
Maana ya neno abdi (Nomino katika ngeli ya [a-/wa-]) (ush) mlimwengu, mja wa Mwenyezi Mungu. Kisawe chake ni abidi. Abdi Katika Kiingereza (English translation) Abdi katika Kiingereza ni: Worshipper, servant of God. Read more
Maana ya neno abakusi na English translation
Maana ya neno abakusi (Nomino katika ngeli ya [i-/zi-]), kifaa chenye shanga au vihesabio vilivyotungwa kwenye nyuzi au nyaya kwa ajili ya kuhesabia. Abakusi Katika Kiingereza (English translation) Abakusi katika Kiingereza ni: Abacus. Read more
Maana ya neno abadi na English translation
Maana ya neno abadi (Kielezi), neno linaloonyesha kutokoma kwa muda; daima, milele. Mfano: Anaishi hapa abadi. Abadi Katika Kiingereza (English translation) Abadi katika Kiingereza ni: Eternal. Read more
Maana ya neno abadani na English translation
Maana ya neno abadani (Kitenzi) neno la kusisitiza jambo lililo- tajwa ambalo limekanushwa. Visawe ni: hata kidogo, katakata, kamwe, asilani, katu. Mfano: Sitakuja kwako abadani. Abadani Katika Kiingereza (English translation) Abadani katika Kiingereza ni: never. Read more
Maana ya neno abaa! na English translation
Maana ya neno abaa! (Kihisishi) neno linalojenga usikivu wa yule unayemwita. Visawe ni: aisee, halo, oha. Abaa! Katika Kiingereza (English translation) Abaa! katika kiingereza linaweza tafsiriwa kama “Hey!” Read more
Maana ya aazi na English translation
Maana ya aazi 1. (Nomino katika ngeli ya [a-/wa-]), ni mtu wa thamani. Visawe ni: mwa- ndani, muhibu. 2. (Kkivumishi) -enye thamani. Kisawe ni bora. Mfano: Fursa niliyopewa ni kitu aazi kwangu. Aazi Katika Kiingereza (English translation) Aazi katika Kiingereza ni: valuable, precious. Read more
Maana ya aathari na English translation
Maana ya aathari Aathari ni nomino katika ngeli ya [i-/zi-], mabaki (yatokanayo) na vitu vya zamani vinavyohusiana na mila, utamaduni na desturi za watu wa jamii fulani. Mfano: makaburi ya wafalme, nyumba, mahekalu, vigae vya vitu vya ufinyanzi n.k. Aathari Katika Kiingereza (English translation) Aathari katika Kiingereza ni “historical remains.” Read more
Maana ya aalimu na English Translation
Aalimu ni nomino katika ngeli ya [a-/wa-] Wingi wa aalimu ni maalimu. Neno aalimu linatumika katika muktadha wa dini. Maana ya aalimu 1. Aalimu ni mtu aliye- bobea katika elimu dini ya Kiislamu. 2. (kama kivumishi) mwenye elimu kubwa ya dini ya Kiislamu. Aalimu Katika Kiingereza (English translation) Aalimu katika kiingereza anaweza tafsiriwa kama “Islamic… Read more