Vitendawili na majibu
1. Adui lakini po pote uendako yuko nawe. Inzi
2. Afahamu kuchora lakini hajui achoracho. Konokono
3. Afuma hana mshale. Nungunungu
4. Ajenga ingawa hana mikono. Ndege
5. Ajifungua na kujifunika. Mwavuli
Soma zaidi hapa: https://mhariri.com/kamusi/vitendawili-vya-kiswahili-na-majibu-yake/
Hizi hapa ni vitendawili:
- Akitokea watu wote humwona. Jua
- Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni. Ugonjwa
- Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza. Mgomba
- Alipita mtu ana bunda la mshale. Mkindu
- Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo. Inzi
soma zaidi: https://mhariri.com/kamusi/vitendawili-vya-kiswahili-na-majibu-yake/
F
1. Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani. Mwezi na nyota angani
2. Fika umwone umpendaye. Kioo
3. Fuko kajifukia, mkia kaacha nje. Kata mtungini
4. Funga mizigo twende Kongo. Mikia ya mbwa
B
1. Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali. Muwa
2. Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea. Sisimizi
4. Babako akojoapo hunung’unika. Mawingu
5. Babu amefunga ushanga shingoni. Mtama/Nazi
6. Babu anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe. Muwa
7. Babu hupiga kelele akojoapo. Mvua
8. Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo. Mti na shoka
9. Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi? Siafu
10. Bak bandika, bak bandua. Nyayo
11. Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani. Mlango
12. Bibi kikongwe apepesa ufuta. Kope za macho
13. Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroMoyoKinu cha kutwangia
Mifano ya Vitendawili ni kama:
Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo. Pazia
Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka. Mjusi/Panya
Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana. Dunia na mbingu
Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe. Jani likwanyukapo
Dada yangu kaoga nusu. Jiwe mtoni
Drrrrrh1 Ng’ambo. Daraja la buibui