Notifications
Clear all

Taja aina za vihusishi na mifano

   RSS

0
Topic starter

aina za vihusishi na mifano

4 Answers
0

Aina za vihusishi na mifano

1. Vihusishi vya wakati
Mifano:
a. Tangu Mwaliko ashindwe uchaguzi hakuzungumza mtandaoni.
b. Nitaendelea kuwafunza Kiswahili hadi tufanikiwe.
c. Baada ya kuhitimu uandishi nitajiunga na sanaa ya uigizaji.
d. Jeupe alibeba mizigo mpaka akachoka.
e. Kabla ya kumwona Atieno, nilimchumbia Awino.
f. Toka nichelewe kufikia malengo yangu, niliamua kutokufa moyo.
Vihusishi vya wakati: tangu, hadi, baada ya, mpaka, kabla ya, toka.
2. Vihusishi vya mahali.
Mifano:
a. Tulimwona Juma katika shamba lake.
b. Kima alipanda juu ya mti.
c. Mtemi Zedekaya ameketi kando ya Nina.
d. Mzee Kengi amelala chini ya mbuyu.
e. Panya ameingia ndani ya gunia.
f. Kifaranga amejificha mvunguni mwa kitanda.
Vihusishi vya mahali: katika, juu ya, kando ya, chini ya, ndani ya, mvunguni mwa.
3. Vihusishi vya kiwango.
– Hivi huhusisha vitu kwa kuvilinganisha labda kwa kutegemea uzito, nguvu au kufaulu.
Mifano:
a. Kilo hamsini za sukari ni zaidi ya kilo tatu za chumvi.
b. Kiptum alikimbia mithili ya duma.
c. Ekari kumi za shamba ni sawasawa na shilingi milioni ishirini.
d. Kati ya elimu na pesa, ni gani bora?

0

Aina za vihusishi ni:

Vihusishi vya Mahali

Mfano: mbele ya, nyuma ya, chini ya, kando ya, karibu na, mbali, mbele ya,ndani ya, na n.k.

Vihusishi vya Wakati

Mfano: baada ya, kabla ya,baada ya, tangu,mnamo n.k.

Vihusishi vya kinyume

Mfano: licha ya,badala ya, bila n.k.

Vihusushi vya kufananisha

Mfano: mithili ya, tamthili ya, kama, mfano wa n.k.

Vihusishi vya a- unganifu

Mfano: cha, pa, vya n.k.

Vihushishi vya sababu

Mifano: kwa kuwa, kwa sababu, kwa vile n.k.

Vihushishi vilinganishi / Vya ulinganifu

Mfano: kuliko n.k.

Vihisishi vya kuonyesha hali

Mfano; sawa na, kwa niaba ya,miongoni mwa,kwa minajili ya n.k.

 

 

 

 

0

Aina za Vihusishi

Vihusishi vya Mahali

Mfano: mbele ya, nyuma ya, chini ya, juu ya, kando ya, karibu na, mbali na.

Vihusishi vya Wakati

kabla ya, baada ya.

0

Aina kuu za vihusishi ni:

1. Vihusishi vya Wakati:

Huonyesha uhusiano wa wakati kati ya matukio mawili.
Mifano: tangu, hadi, baada ya, mpaka, kabla ya, toka
2. Vihusishi vya Mahali:

Huonyesha uhusiano wa mahali kati ya vitu viwili.
Mifano: katika, juu ya, kando ya, chini ya, ndani ya, mvunguni mwa
3. Vihusishi vya Kiwango:

Hulinganisha vitu kwa kutegemea uzito, nguvu, au kufaulu.
Mifano: zaidi ya, mithili ya, sawa na, badala ya, kuliko