Mhariri Forum

Notifications
Clear all

Taja mifano ya nomino ambata

   RSS

0
Topic starter

mifano ya nomino ambata

4 Answers
0

Nomino ambata huuundwa kwa nomino mbili (majina mawili) ambazo huambatanishwa na kuwa neno moja. Aghalabu maneno yanayounganishwa hayana uhusiano wowote kimaana.

Mifano

  • Askari + kanzu = askarikanzu
  • mwana + mkiwa = mwanamkiwa
  • Mwana +nchi = mwananchi
  • Mbwa + mwitu = mbwamwitu
  • Pembe + tatu = pembetatu
  • Kiinua + mgongo = kiinuamgongo
  • Nusu + kipenyo = nusukipenyo
  • Simba + marara = simbamarara
0

Mifano ya nomino ambata:

1. Mwana + jeshi -> mwanajeshi

2. Mwana + riadha -> mwanariadha

3. Mwana + mbee -> mwanambee

4. Mja + mzito -> mjamzito

5. Mla + riba -> mlariba

0

Mifano ya nomino ambata:

  • Mwana + mwali -> mwanamwali
  • Kifungua + mimba -> kifunguamimba
  • Mweka + hazina -> mwekahazina
  • Mchanja + kuni -> mchanjakuni
  • Mwana + funzi -> mwanafunzi
0

Mifano ya nomino ambata katika sentensi

  • Mwanajeshi jasiri alilinda nchi yake kwa ujasiri.
  • Mwanariadha mwenye kasi alishinda mbio kwa urahisi.
  • Mjamzito alihisi mtoto wake akicheza tumboni.
  • Mwanamwali mrembo alivutia macho ya kila mtu.
  • Mwekahazina alihakikisha usalama wa mali ya kampuni.