Notifications
Clear all

Taja mifano ya semi na maana zake

   RSS

0
Topic starter

mifano ya semi na maana yake

4 Answers
0

Mifano ya semi na maana

1.Kiguu na njia-Mja asiyetulia.
2.Kuwa kupe au mnyonyaji-Kutegemea jasho la watu
3.Kanyaga chechele-Kusahau au kupotea njia.
4.Kula vya mwiku-Kula chakula kilicholala.
5.Daiwa kope si zake-Kuwa na madeni mengi.

0

Mifano ya semi ni:

Kula mwata-Pata taabu.
Kula mwande-Kosa ulichokitarajia.
Kula kalenda-Fungwa gerezani.
Chezea shere-Dhihaki;fanyia mzaha.
Kata kalima-Katiza mtu usemi.

0
  • Kucheza ngoma goya-Fanya jambo lisilo na faida.
  • Ng’oa nanga/Tweka nanga-Anza safari.
  • Jipalia makaa kama pweza-Jitia mashakani.
  • Kubali shingo upande-Kubali bila kupenda.
  • Kazi ya kijungu jiko-Kazi ya kujipa riziki tu.
0

Mifano ya semi au nahau:

  • Kunja jamvi-Maliza shughuli.
  • Kula chumvi nyingi-Zeeka,ishi miaka mingi.
  • Zunguka mbuyu-Honga au hongwa.
  • Kula yamini-Apa.
  • Ifa fa ima-Kwa vyovyote vile.
  • Kuvaa miwani-Kulewa.
  • Kijibwa na bwanashamo-Kufuatana.
  • Kula njama-Fanya mkutano wa Siri wenye nia mbaya.
  • Changa bia/ubia-Shirikiana.