ngeli za kiswahili na mifano yake
Mifano ya nomino katika ngeli ya A – WA:
- Wanadamu: mtoto, ndugu, msamaria, daktari, kiongozi
- Wanyama: ng’ombe, mbuzi, swara, nyati, nguchiro
- Ndege: bata, kuku, njiwa, mwewe, kipanga
Ngeli ya I-ZI
Haya ni majina ya vitu visivyokuwa na uhai .
Nomino katika ngeli hii huchukua I kwa umoja na ZI kwa wingi
Mifano ya nomino katika ngeli hii ni: Dawa, saa, ndizi, redio, ngoma, nyumba, chupa, radi na kadhalika.
Mifano katika sentensi.
1)Ngoma hii haipendezi (umoja). Ngoma hizi hazipendezi. (wingi)
2)Dawa hii inanidhuru (umoja). Dawa hizi zinadhuru (wingi)
3)Chupa imevunjika (umoja). Chupa zimevunjika (wingi)
NGELI YA U-ZI
Majina katika ngeli hii huhusisha vitu vyembamba na virefu ,yenye wingi wa ‘ny’ au ‘m’ au ‘nd’ ambayo yanatumia upatanisho wa kisarufi wa ‘u’.
Mifano ya majina katika ngeli hii:
1) Ukucha
2) Ulimi
3) Ukuta
4) waya
5) Ufa
6) Ubawa
7) Wimbo
8) Wakati
Ngeli ya LI-YA
Inahusisha nomino zinazoanza kwa “Ji” katika umoja na “Ma” katika wingi.
Mifano:
Jino limeng’oka (Umoja) – Meno yameng’oka (Wingi)
Jicho limevimba (Umoja) – Macho yamevimba (Wingi)
Tunda limeoza (Umoja) – Matunda yameoza (Wingi)
Ngeli ya KI-VI
Ngeli ya KI-VI inatumiwa kuashiria hasa viumbe visivyo na uhai.
Mfano:
Kijiko «ki»mepotea.
Vijiko «vi»mepotea.
Ngeli ya U-U
Mfano:
Ukaidi wake «u»limchongea.
Ukaidi wao «u»liwachongea.
Ngeli ya U-YA
Huwa na majina ya hali, matendo, na kadhalika. Kiambishi {–u} katika umoja na {–ya} katika wingi hutumika katika upatanisho wake wa kisarufi.
Mfano:
Upishi wake «u»mewavutia.
Mapishi yake «ya»mewavutia.
Ngeli ya YA – YA
Mfano:
Mafuta
Maarifa
Mazingaombwe
Maasi
Mamlaka
Makala n.k.