mifano ya vivumishi
Vivumishi vya sifa
Hutoa sifa juu ya nomino.
Kuna:
Vivumishi vinavyochukua viambishi ngeli:
Mifano:
▪Mtoto «mnene» amelia.
▪Miti «mirefu» imekatwa.
Vivumishi visivyochukua viambishi ngeli:
Mifano:
▪Mchezaji «stadi» hupendwa.
▪Tulipewa mifano «tele».
Mfano wa vivumishi vya idadi
Kuna aina mbili za vivumishi vya idadi.
a) Idadi Kamili
Hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino.
Kwa mfano: tatu, mbili, kumi
Msichana mmoja amewauwa nyoka wawili
Siku kumi zimepita tangu Bi Safina alipojifungua watoto watatu
b) Idadi Isiyodhihirika
Huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja idadi kamili
Kwa mfano: chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani
Vivumishi viunganifu -a-
Ni vijineno vinavyotokana na kuambatanisha -a- na viambishingeli ili kuleta maana na uhusiano unaodhamitiwa.
Mifano ya vivumishi viunganifu -a- ni;
la, wa, ya, za, cha,pa, vya mwa, kwa
Vivumishi vya idadi hutumika kuonyesha kiasi au idadi ya vitu au watu. Aina kuu mbili za vivumishi vya idadi ni:
1. Idadi kamili:
Hizi huonyesha idadi maalum ya vitu au watu.
Mifano:
Wakulima wanne wamepewa tuzo.
Viti kumi na saba vimeletwa.
2. Idadi isiyodhihirika:
Hizi huonyesha kiasi kisichojulikana cha vitu au watu.
Mifano:
Wanafunzi wachache hawakufaulu.
Nyumba nyingi zimebomolewa.