mifano ya vivumishi vya nomino
Vivumishi ni vya aina kumi:
– Vivumishi vya sifa
– Vivumishi vya idadi
– Vivumishi visisitizi
– vivumishi vimilikishi
– Vivumishi virejeshi
– Vivumishi vionyeshi
– Vivumishi vya a- unganifu
– Vivumishi vya nomino kwa nomino.
– Vivumishi vya pekee
– Vivumishi viulizi
Mifano ya vivumishi
– Vivumishi vya sifa
Mfano: kizuri, kali, safi, mrembo
– Vivumishi vya idadi
Mfano: tatu, mbili, kumi, chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani
– Vivumishi visisitizi
Mfano: yuyu huyu, wawa hawa, kiki hiki, papo hapo, mumu humu
– vivumishi vimilikishi
Mfano: changu, lako, yake, kwetu, vyenu, zao
– Vivumishi viulizi
Mfano: -ngapi?, -pi?
1. Vivumishi Visisitizi
Husisitiza nomino fulani kwa kurudia rudia
k.m:
- Jahazi lili hili
- Wembe ule ule
- Ng’ombe wawa hawa
2. Vivumishi Viashiria / Vionyeshi
Vivumishi viashiria hutumika kuonyesha au kuashiria nomino kulingana na mahali.
Mfano: Karibu hapa, huyu, hiki, hili, huku, haya, ule, wale, pale, Mbali kidogo hapo, huyo, hiyo, hicho
Vivumishi visisitizi
Mfano: yuyu huyu, wawa hawa, kiki hiki, papo hapo, mumu humu
Vivumishi vimilikishi
Mfano: changu, lako, yake, kwetu, vyenu, zao