Loyal in Swahili (English to Swahili Translation)

Posted by:

|

On:

|

Definition of loyal in English

Loyal is giving or showing firm and constant support or allegiance to a person or institution.

Loyal in Swahili

Loyal in Swahili is -aminifu.

Maana ya -aminifu katika Kiswahili

-aminifu ni kutenda jambo vile ulivyoagizwa. (doing what you were instructed to do.)

Examples of loyal in Swahili in sentences

 • Sijisikii mwaminifu kwa kampuni hii tena. (I don’t feel loyal to this company any longer.)
 • Wamebakia kuwa waaminifu kwa rais. (They had remained loyal to the president.)
 • Alikuwa mwaminifu kwa nchi yake. (He was loyal to his country.)
 • Jack amekuwa mfanyakazi mwaminifu katika kampuni hii kwa karibu miaka 50. (Jack has been a loyal worker in this company for almost 50 years.)
 • Alikuwa mtumishi wa umma mwaminifu, mashuhuri na mwenye uwezo mkubwa. (He was a loyal, distinguished and very competent civil servant.)
 • Wanajeshi waaminifu walianzisha mashambulizi ya kukabiliana na waasi. (Loyal armed forces launched a counter-attack against the rebels.)
 • Wanajeshi walibaki waaminifu kwa rais. (The troops remained loyal to the president.)
 • Zuri alikuwa rafiki yake wa kudumu na mwaminifu. (Zuri was her constant friend and loyal.)
 •  Yeye ni mwaminifu na anategemewa kabisa. (He is loyal and totally dependable.)
 • Ni rafiki mwaminifu.( She is a loyal friend.)
 • Daima amebaki mwaminifu kwa kanuni zake za kisiasa. (She has always remained loyal to her political principles.)
 •  Alibaki mwaminifu kwangu katika hali ngumu na mbaya. (He remained loyal to me through thick and thin.)
 • Walikuwa waaminifu bila kuyumbayumba kwa marafiki zao. (They were unflinchingly loyal to their friends.)
 • Yeye ni mwaminifu sana kwa marafiki zake. (She’s very loyal to her friends.)
 • Ninamhukumu kuwa mwaminifu. (I judge him to be loyal.)
 • Watu walibaki waaminifu kwa nchi yao. (The people stayed loyal to their country.)
 • Daima amekuwa rafiki mwaminifu kwetu sote. (He’d always been such a loyal friend to us all.)
 •  Rafiki zake wengine wote walipomwacha, Steve aliendelea kuwa mwaminifu. (When all her other friends deserted her, Steve remained loyal.)
 • Yeye ni rafiki yangu mwaminifu. (She’s a loyal friend of mine.)
 •  Mbwa ni wanyama waaminifu. (Dogs are loyal animals.)