Maana ya neno ambua na English translation

Posted by:

|

On:

|

Maana ya neno ambua

Matamshi: /ambua/

(Kitenzi elekezi )

Ambua 1

1. ondoa ganda la juu. Kisawe chake ni menya.

2. fanikiwa au faidika. Kisawe chake ni zawadiwa.

Mnyambuliko wa ambua ni: → ambulia, ambulika, ambulisha, ambuliwa.

Ambua 2

(Kitenzi elekezi)

Maana: nyanyua; inua, vuta juu.

Mnyambuliko wake ni: → ambuana, ambulia, ambulika, ambulisha, ambuliwa.

Ambua Katika Kiingereza (English translation)

Ambua katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

  • Ambua (ondoa ganda la juu) ni: peel, shell.
  • Ambua (fanikiwa au faidika) ni: succeed, benefit or be rewarded.
  • Ambua (nyanyua; inua, vuta juu) ni: lift or pull up.