Tofauti kati ya nomino za pekee na nomino za kawaida

Posted by:

|

On:

|

Nomino za pekee

Nomino za pekee ni maneno yanayotaja majina mahususi ya watu, mahali, au vitu ambavyo vina sifa ya pekee. Nomino za pekee huanza kwa herufi kubwa.

Mifano ya nomino za pekee:

Watu: John, Mary, Barack Obama, Nelson Mandela

Maeneo: Dar es Salaam, Nairobi, London, New York

Vitu: Mwezi, Jua, Dunia, Bahari

Mifano ya nomino za pekee katika sentensi

i)     Mto Nzoia hufurika wakati wamasika.

ii)    Paulo ameenda sokoni sasa hivi.

iii)   Nairobi ndio mji mkuu wa Kenya.

iv)   Ziwa Bogoria hupatikana katika eneo la Bonde la Ufa.

Nomino za kawaida

Nomino hizi hutaja vitu kwa kawaida. Nomino hizi hurejelea dhana ,vitu  au viumbe vinavyopatikana duniani. Mfano wa nomino za kawaida ni mtu,kitu,jino,redio,runinga,ukuta.

Hizi ni nomino ambazo hazianzi kwa herufi kubwa ila tu zinapotumika mwanzoni mwa sentensi k.m.

i)     Wanafunzi walishirikishwa kupanda miti mwaka huu.

ii)    Wanafunzi watazuru ikulu ya raisi hiyo kesho.

iii)   Wananchi hupaswa kutii sheria za nchi kila mara.