ngeli ya PA/KU/MU
Ngeli hii, inayojulikana kama Ngeli ya Mahali, hufafanua matumizi ya viambishi “-pa-“, “-ku-“, na “-mu-” katika sarufi ya Kiswahili. Viambishi hivi hutumika kuonyesha mahali pa nomino.
Nomino zingine zinazoainishwa katika ngeli hii ni pamoja na “mahali” na “pahali.” Nomino za kawaida zinapoongezwa kiambishi tamati “-ni,” huainishwa katika Ngeli ya Mahali.
Mfano:
Usoni
Shuleni
Moyoni
Makundi Matatu ya Ngeli ya Mahali:
Ngeli ya Mahali imegawanywa katika makundi matatu makuu yanayoonyesha mahali maalum kwa mujibu wa nomino husika:
1. PA-PA:
Kundi hili linaonyesha mahali dhahiri, panapoonekana wazi.
Mfano:
Usoni pake pana tabasamu la daktari.
Nyusoni mwao pana tabasamu la daktari.
Kichwani pake pana kofia nyeupe.
Vichwani mwao pana kofia nyeupe.
2. KU-KU:
Kundi hili linaonyesha mahali kulikosiringirwa, mahali kusikodhihirika.
Mfano:
Shuleni kwangu kuna mwalimu stadi.
Shuleni kwetu kuna walimu stadi.
Uwanjani huko uendako kuna mchezo.
Nyanjani huko mwendako kuna michezo.
3. MU-MU:
Kundi hili linaonyesha mahali mlimo ndani, yaani undani wa kitu fulani.
Mfano:
Moyoni mwangu mna raha.
Mioyoni mwetu mna raha.
Garini humu mna mzigo mzito.
Magarini humu mna mizigo mizito.
PA (mahali karibu au panapodhihirika) k.m. Kitabu kipo pale.
KU (mahali mbali au kusikodhihirika) k.m. Mahali kule kunafaa.
MU (ndani ya) k.m. Mahali mle mna siafu.
Mfano wa majina katika hii ngeli ni: Hekaluni,msikitini,mahegeshoni,shimoni, mkobani, sebuleni, uwanjani, chumbani, darasani, kaburini, nk.
Mfano: shuleni, pangoni, jikoni, shambani nk