Notifications
Clear all

Mifano ya nomino katika ngeli ya i-zi ni?

   RSS

0
Topic starter

nomino katika ngeli ya i-zi

4 Answers
0

Ngeli hii inajumuisha nomino za vitu visivyo na uhai.

Nomino hizi umoja na wingi wake huwa ni sawa. 

Mfano wa nomino katika ngeli ya I-ZI ni: kalamu, meza, sahani, rafu, linga, saa, rula, nyumba, soksi, karatasi, linga, kamusi, wiki, siku, chaki, chupa, ndizi, kamba, bawaba, pete n.k.

0

Mifano ya majina katika ngeli ya i-zi ni kama vile: nyumba, nguzo, njia, nafasi, nyota, nyama, ndoo, ndizi, n.k. 

0

Kwa mara nyingi nomino katika ngeli hii huanza na herufi ‘n’ na wingi wake hubadiliki.

Mfano:

Nyanya, Nchi, Nyundo, Nyika, Ngano, Njaa, Njia, Nafaka, Nta, Ndoa, Ngozi, n.k.

0

Baadhi ya nomino katika ngeli hii zilizotoholewa kutoka lugha ngeni.

mifano ni kama: kalamu, meza, redio, karatasi, taa, barua n.k.