mifano ya vivumishi
Vivumishi hutoa maelezo kuhusu nomino.
Mifano:
– Mtu «mzuri».
– Kisu «kikali».
Kivumishi ni neno linalo zungumzia zaidi kuhusu nomino k.m msichana mrembo ameolewa. Neno mrembo linazungumzia zaidi kuhusu msichana. Hivo basi neno mrembo ni kivumishi.
Vivumishi vya sifa
Vivumishi vya sifa ambavyo vina mizizi inayoanza na irabu huchukua kiambishi «j-» katika umoja na «ma-» kwa wingi.
Na ikiwa ni kivumishi chenye mzizi unaoanza na irabu, huchukua kiambishi «ji-» kwa umoja lakini «ma-» kwa wingi.
Mifano :
– Tumbo lake ni «jembamba» (Matumbo yao ni «membamba»).
– Jino «jeupe refu» ndilo litang’olewa (Meno «meupe marefu» ndiyo yatang’olewa).
– Amenunua jembe «jipya kali» (Amenunua majembe «mapya makali»).
– Agano «jipya» (Maagano «mapya»).
Aina za vivumishi_____vya sifa…baya,zuri,Safi nk
_vya pekee…..ote, oote,enye,enyewe,ingine,ingineo.
_vivumishi vimilikishi ….angu,etu,ako,enu,aje,so.
__vya idadi….Kuna idadi kapa/tasa na zisizokapa yaani kapa haichukui kiambishi ngeli mf sits,Saba,Tisa,kumi.Piakuna idadi bainifu na zisizo bainifu yaani zinazo hesabika na zisizohesabika/jumla_mf chache,info kadhaa,tele,foko nk
__vivumishi viashiria(kuashiria ni kuonyesha)tunaashiria Hali tatu____hapa,hapo,pale au karibu,mbali kidogo,mbalisana mifano_ngeli a_wa huyu,huyo,yule.
__vivumishi visisitizi(kutilia mkazo)..mf..yuyuhuyu.
__vivumishi viradidi(kurudiarudia)mf…huyuhuyu.
__vivumishi viulizi…..mf…gani,ngapi ,_pi. Gani ni kapa na ngapi hutumika katika wingi.
__vivumishi vya a unganifu …mf cha,la,kwa,la,za,ya,nk.
__vivumishii vya nomino. Hii no nomino inayoeleza zaidi kuhusu nomino nyingine …mf…mama mzazi,mama msusi,askali kijana nk nomino ya pili ni kivumishi.
__vivumishi virejeshi….mf o rejeshi na amba.