Mhariri Forum

Notifications
Clear all

Taja mifano ya vitanza ndimi

   RSS

0
Topic starter

mifano ya vitanza ndimi

4 Answers
0

Mifano ya vitanza ndimi

  • Kanga wa mahanga mwenye matanga anatangatanga tanga.
  • Mchuuzi wa mchuzi wa juzi hajui mjusi wa jana.
  • Katika kata ya mitakataka mkuu wa kata alikataa katakata takataka zisitupwe pahali tambarare tena.
0

Hizi hapa ni mifano ya vitanza ndimi:

  • Shirika la reli la Seychelles lilishirikiana na shirika la reli la Senegal.
  • Wape wale wanawali wale wali wao.
  • Pema ni pema hujapopema ukipema si pema tena.
  • Ni Nini kikusikitishacho?
0

Mifano ya vitanza ndimi ni:

  • Msasa wa sasa wa Sasha una mkasa wa kasa si kasha.
  • Susumila Shushushu mwenye sunzu si zuzu ila ana susu yenye shushu na ni chuchu.
  • Ukivumbua alichovumbua Wambua akila kitumbua bila kukichambua sitakusumbua tena.
0
  • Usishangae kama shangazi aliye nunua shanga kwa bei ya kushangaza.
  • Wataita wa Taita wataita Wataita wa Taita.
  • Sitasita kusisitisa kuwa sita na sita si tisa.
  • Paliondokea mamba aliejibamba na kujigamba katika magamba ya wakamba huko ukambani.