Mhariri Forum

Notifications
Clear all

Ni zipi baadhi ya njia za kujua ikiwa mtu mwingine anavutiwa nawe?

   RSS

0
Topic starter

Tupe Nbaadhi ya njia za kujua ikiwa mtu anapendezwa nawe.

@derrick mara nyingi unaweza kujua kwa kutilia maanani tabia zake wakati manazungumza ama kuhusiana.

4 Answers
0

Wanajibu haraka kwa meseji au simu zako.
Ikiwa mtu anavutiwa nawe, atajibu jumbe au simu zako kwa haraka zana, kwa sababu anataka kuanzisha mazungumzo nawe ili apate kukujua zaidi.

0

Kama anazungumzia kila wakati juu ya kupanga kukutana nawe. Mkiwa pamoja mnafurahia—sio tu kuangalia movies kila wikendi—na wanatumia muda huo kufahamiana. Mtu akivutiwa nawe hayuko tayari kuwasiliana naye kupitia simu au ujumbe mfupi tu, lakini pia ako tayari kutenga muda wa kukutana nawe ana kwa ana.

0

Kukuuliza maswali kukuhusu huonyesha kwamba mtu amevutiwa nawe na anataka kukujua zaidi. Kama mtu amevutiwa nawe anakuuliza maswali ya kimantiki, na ingawa hakuna ubaya na mazungumzo madogo, maswali hayo labda sio “Unafanya nini wikendi hii?” au “Unapenda kufanya nini ili kujifurahisha?” Badala yake, anakuuliza maswali ya ndani zaidi, na yanaweza kuhusisha malengo na maadili yako ya baadaye. Aina hiyo ya maswali na mazungumzo yanaonyesha kwamba mtu anaenda mbali zaidi ya kukujua kama mwenza.

0

Kukutazama kwa macho ni kidokezo kuwa anavutiwa nawe sana. Wanaume na wanawake wote watatumia macho wakati wanapenda mtu. Ikiwa mtu anakupenda basi atakuangalia mara nyingi zaidi.