Mistari ya biblia kuhusu baraka

Posted by:

|

On:

|

Mungu huwabariki wale wanaompenda. Anatutunza kila wakati wa maisha yetu. Yeyote anayemtii Mungu anambarikiwa na atapata baraka kuu kutoka kwa mungu nayo ni “uzima wa milele”.

Mungu pia anatuita tuwabariki watu wengine. Yeyote anayembariki mtu anamtakia mema. Ni lazima tuwabariki hata adui zetu!

Hizi hapa ni mistari ya biblia kuhusu baraka, kukusaidia kupata baraka kutoka kwa Mungu na kuwabariki watu wengine.

Mistari ya biblia kuhusu baraka

Yeremia 17:7 SRUVDC (SRUVDC: Swahili Revised Union Version)

Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.

Hesabu 6:24-26 NEN (NEN: Neno: Bibilia Takatifu)

“BWANA akubariki na kukulinda; BWANA akuangazie nuru ya uso wake na kukufadhili; BWANA akugeuzie uso wake na kukupa amani.” 

Mithali 10:22 SRUV

Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.

Zaburi 32:1 BHN ( BHN: Biblia Habari Njema)

Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake, mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.

Zaburi 119:2 BHN

Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote.

Zaburi 33:12 BHN

Heri taifa ambalo Mungu wake ni Mwenyezi-Mungu; heri wale aliowachagua kuwa watu wake mwenyewe!

Zaburi 29:11 BHN

Mwenyezi-Mungu na awape watu wake nguvu! Mwenyezi-Mungu na awabariki watu wake kwa amani!

Zaburi 128:1-4 BHN

Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu, wanaoishi kufuatana na amri zake. Utapata matunda ya jasho lako, utafurahi na kupata fanaka. Mkeo atakuwa kama mzabibu wa matunda mengi nyumbani mwako; watoto wako kama chipukizi za mzeituni kuzunguka meza yako. Naam, ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Mwenyezi-Mungu.

Waefeso 1:3 SRUV

Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo.

Zaburi 91:2 BHN

ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu: “Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu; Mungu wangu, ninayekutumainia!”

Mithali 3:13 SRUV

Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.

1 Petro 1:3 NEN

Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema zake kuu ametuzaa sisi mara ya pili katika tumaini lenye uzima kupitia kwa kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu.

Mika 6:8 BHN

Mungu amekuonesha yaliyo mema, ewe mtu; anachotaka Mwenyezi-Mungu kwako ni hiki: Kutenda mambo ya haki, kupenda kuwa na huruma, na kuishi kwa unyenyekevu na Mungu wako.

Zaburi 23:1-6 SRUV

BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Yakobo 1:12 – Bibilia Takatifu

12 Amebarikiwa mtu ambaye anavumilia majaribu, kwa sababu akisha stahimili atapewa taji ya uzima ambayo Mungu amewaahidi wale wampendao.

Mathayo 5: 3-11 BHN

3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

5 Heri walio wapole, maana watairithi nchi.

6 Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

7 Heri walio na huruma, maana watahurumiwa.

8 Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu.

9 Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.

10 Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

11“Heri yenu nyinyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu. 12 Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu.

Zaburi 1:1-2 BHN

Heri mtu asiyefuata shauri la waovu, asiyeshiriki njia za wenye dhambi, wala kujumuika na wenye dharau; bali huifurahia sheria ya Mwenyezi-Mungu, na kuitafakari mchana na usiku.

2 Wakorintho 1:3 BHN

Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba mwenye huruma na Mungu mwenye kuleta faraja yote.

Wafilipi 4:19 SRUV

Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

Zaburi 146:5 BHN

Heri mtu anayesaidiwa na Mungu wa Yakobo, mtu aliyeweka tumaini lake kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wake