Category: Maana ya maneno

  • Maana ya neno aminifu na English translation

    Maana ya neno aminifu Matamshi: /aminifu/ (Kivumishi) Maana: sifa ya mtu asiyesema uwongo au kudanganya; yenye kusadikika au kubalika. Aminifu Katika Kiingereza (English translation) Aminifu katika Kiingereza ni: honest, trustworthy. Read more

  • Maana ya neno amini na English translation

    Maana ya neno amini Matamshi: /amini/ Amini 1 (Kitenzi elekezi) Maana: 1. sadiki au kubalia ukweli wa kitu au jambo. 2. kubali kuwa fulani anakubalika. Mfano: Juma hakuniangusha tamashani ndiyo maana ninamuamini. Mnyambuliko wa amini ni: → aminia, aminiana, aminika, aminisha, aminiwa. Amini 2 (Kitenzi elekezi) Maana: sadiki na tekeleza mafunzo ya dini. Mfano: Dini… Read more

  • Maana ya neno amin! na English translation

    Maana ya neno amin! Matamshi: /amin/ (Kihisishi) Maana: pia amina! Kiitikio cha kuitika maombi au ibada kama vile kanisani au msikitini kumaanisha iwe hivyo. Amin Katika Kiingereza (English translation) Amin katika Kiingereza ni: amen. Read more

  • Maana ya neno amilisha na English translation

    Maana ya neno amilisha Matamshi: /amilisha/ (Kitenzi si elekezi) Maana: hatua inayotoa kibali cha kuanza kwa mchakato wa matumizi kwenye tarakilishi au simu. Mnyambuliko wake ni: → amilishia, amilishika, amilisha, amilishiwa. Amilisha Katika Kiingereza (English translation)  Amilisha katika Kiingereza ni: launch, open, initiate or start. Read more

  • Maana ya neno amili na English translation

    Maana ya neno amili Matamshi: /amili/ Amili 1 (Kitenzi elekezi) Maana: jua, fahamu, maizi, tambua, ng’amua, elewa. Mnyambuliko wake ni: →amilia, amiliana, amilika, amilisha, amiliwa. Amili 2 (Kitenzi elekezi) 1. tenda kazi au shughuli. Kisawe chake ni shughulika. 2. unda au tengeneza. 3. karabati au rekebisha kitu kilichoharibika. Mnyambuliko wake ni: → amilia, amiliana, amilika,… Read more

  • Maana ya neno amikto na English translation

    Maana ya neno amikto Matamshi :/amiktɔ/ (Nomino katika ngeli ya [i-zi]) Maana: kitambaa cheupe cha katani kinachotandwa mabegani na padri wa kanisa Katoliki kabla ya kuvaa nguo nyingine rasmi za misa. Amikto Katika Kiingereza (English translation) Amikto katika Kiingereza ni: amice. Read more

  • Maana ya neno amidi na English translation

    Maana ya neno amidi Matamshi: /amidi/ (Kitenzi elekezi) Maana: 1. fikia maamuzi au kata shauri. 2. tegemea au tarajia kupata mafanikio fulani. Mnyambuliko wake ni: → amidia, amidiana, amidika, amidisha, amidiwa. Amidi Katika Kiingereza (English translation) Amidi katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia: Read more

  • Maana ya neno amiba na English translation

    Maana ya neno amiba Matamshi/amiba/ (Nomino katika ngeli ya [a-wa]) Maana: vidudu vidogo vilivyo hai vyenye seli moja na umbo lao hubadilika wakati wote. Amiba Katika Kiingereza (English translation) Amiba katika Kiingereza ni: Amoeba. Read more

  • Maana ya neno amia na English translation

    Maana ya neno amia Matamshi: /amia/ (Kitenzi elekezi) Maana: linda au kinga shamba la nafaka kwa kutoa kelele inayowatisha na kuwafurusha wanyama waharibifu. Mnyambuliko wake ni: → amilia, amiliana, amilika, amilisha, amiliwa. Amia Katika Kiingereza (English translation) Amia katika Kiingereza ni: guard, protect a garden or field from animals and birds. Read more

  • Maana ya neno ami na English translation

    Maana ya neno ami Matamshi: /ami/ (Nomino katika ngeli ya [a-wa]) Maana: pia amu, ndugu wa kiume wa baba. Mfano: Ami yangu akija atatuletea zawadi nyingi. Ami Katika Kiingereza (English translation) Ami katika Kiingereza ni: Uncle (father’s brother). Read more