Kama msichana amekukataa unaweza jaribu tena?
@antonymukuria Kukubaliwa au kukataliwa ni sehemu ya maisha, hasa linapokuja suala la mahusiano au kujaribu kutafuta uhusiano na mtu. Kwa kawaida, ni muhimu kuheshimu jibu la mtu aliyekukataa.
@antonymukuria msichana aliyekuwacha inamaana kuwa yeye hakutaki. haipaswi uharibu wakati wako ukimfuata aliye kukataa kwa sababu moyo wake uko mahali pengine. jishughulishe na umuombe Mwenyezi Mungu akubariki na mpenzi. mapenzi hayaitaji kulazimisha, tafuta anayekutaka pia
@antonymukuria naam. Naeza mjaribu tena sababu aweza kua alikukataa ila tu kujaribu imani yako na mapenzi yako kwake.
Hakika. Iwapo alikataa, inaweza kuwa ni kwa sababu moja au nyingine. Lakini hakuna sababu ya kudhani kuwa alikuwa akidanganya alipokataa na ni jambo la busara kuuliza tena upate uhakika wa mambo.
Kukubaliwa au kukataliwa ni sehemu ya maisha, hasa linapokuja suala la mahusiano au kujaribu kutafuta uhusiano na mtu. Kwa kawaida, ni muhimu kuheshimu jibu la mtu aliyekukataa.
Naam! Naweza jaribu tena baadaye sababu nitaweza kujua ni nini anchokipenda, anachotaka, na anachotamani. So rahizi kujua matakwa ya msichana kwa mkutano moja. Nikipatikana na yeye kwa mara ya pili, itakuwa rahisi kumtongoza kulingana na vipengele anavyopenda.
Sababu pekee ya kujaribu tena itakuwa ikiwa angekuambia moja kwa moja au kukudokeza kwamba atakuwa tayari katika siku zijazo. Vinginevyo, hapana. Endelea na maisha.
Jaribu mara mbili zaidi, fanya wakati umeanzisha urafiki naye na anahisi salama, usikimbilie mambo.
Kwa nini hujaribu tena? Ukikataliwa kataliwa, haja kusumbua mtoto wa watu.