Category: Maana ya maneno
Maana ya neno ambo na English translation
Maana ya neno ambo Matamshi: /ambɔ/ Wingi wa ambo ni maambo. Ambo 1 (Nomino katika ngeli ya [li-ya]) 1. maradhi yanayosambazika. 2. kitu kinachosambaza au kueneza maradhi au ugonjwa fulani kama vile mdudu au maji. Ambo 2 (Nomino katika ngeli ya [li-ya]) Maana: aina ya gluu au kitu kinachonata kama gundi. Ambo Katika Kiingereza (English… Read more
Maana ya neno ambizana na English translation
Maana ya neno ambizana Matamshi: /ambizana/ (Kitenzi elekezi) Maana: pashana habari hasa kwa njia ya usimulizi badala ya uandishi. Ambizana Katika Kiingereza (English translation) Ambizana katika Kiingereza ni: “converse,” “chat,” “discuss,” or simply “talk.” Read more
Maana ya neno ambisha na English translation
Maana ya neno ambisha Matamshi: /ambisha/ (Kitenzi elekezi) Maana: 1. pia ambisa, sogeza na kupanga vitu kwa mkaribiano kama vile kuziweka dau, ngalawa au mashua pamoja ufukweni; funganisha chombo kimoja cha bahari na chombo kingine. 2. ongeza silabi kisarufi kwenye mzizi wa neno. Mnyambuliko wake ni → ambishia, ambishiana, ambishika, ambishwa. Ambisha Katika Kiingereza (English… Read more
Maana ya neno ambilika na English translation
Maana ya neno ambilika Matamshi: /ambilika/ Ambilika 1 (Kivumishi) Maana: sifa ya mtu unayeweza kumshawishi akubali maoni yako au ya wenzako; mwenye uwezo wa kupokea maoni ya wengine. Ambilika 2 (Kitenzi si elekezi) Maana: weza kupokea au kukubali maoni au rai za watu wengine. Ambilika Katika Kiingereza (English translation) Ambilika katika Kiingereza inategemea na maana… Read more
Maana ya neno ambika na English translation
Maana ya neno ambika Matamshi: /ambika/ Ambika 1 (Kitenzi elekezi) Maana: 1. andaa mtego wa samaki kwa nyavu katika maji yenye kina kirefu au maji mafu. 2. tega chambo katika mshipi wa uvuvi. 3. loweka au didimiza majini. Mnyambuliko wake ni: → ambikia, ambikiana, ambikisha, ambikwa. Ambika 2 (Kitenzi elekezi ) Maana: zulia au singizia… Read more
Maana ya neno ambia na English translation
Maana ya neno ambia Matamshi: /ambia/ (Kitenzi elekezi) Maana: dokeza au pasha mtu habari fulani. Kisawe chake ni: fahamisha; julisha. Mfano: Mwalimu alimwambia Juma kuwa alikuwa amefuzu vizuri katika mtihani wake. Mnyambuliko wake ni: → ambiana, ambika, ambilia, ambiwa, ambiza. Ambia Katika Kiingereza (English translation) Ambia katika Kiingereza ni: To tell or inform someone of… Read more
Maana ya neno ambatisha na English translation
Maana ya neno ambatisha Matamshi: /ambatisha/ (Kitenzi elekezi ) Maana: bandika au ongeza kibandiko kingine cha ziada. Mnyambuliko wa ambatisha ni: → ambatishana, ambatishia, ambatishika, ambatishwa. Ambatisha Katika Kiingereza (English translation) Ambatisha katika Kiingereza ni: To stick or add an additional label. Read more
Maana ya neno ambatano na English translation
Maana ya neno ambatano Matamshi: /ambatanɔ/ Wingi wa ambatano ni maambatano. (Nomino katika ngeli ya [li-ya]) Maana: tendo la kuambatana. Ambatano Katika Kiingereza (English translation) Ambatano katika Kiingereza ni: the act or state of cohering, uniting, or sticking together. Read more
Maana ya neno ambatanisho na English translation
Maana ya neno ambatanisho Matamshi: /ambatanisɔ/ (Nomino katika ngeli ya [i- zi]) Maana: faili au data inayojumuishwa na baruapepe. Ambatanisho Katika Kiingereza (English translation) Ambatanisho katika Kiingereza ni: File or data attached to an email. Read more
Maana ya neno ambatanifu na English translation
Maana ya neno ambatanifu Matamshi: /ambatanifu/ (Kivumishi) Maana: -enye upatanifu au kushikamana. Ambatanifu Katika Kiingereza (English translation) Ambatanifu katika Kiingereza ni: have harmony or cohesion. Read more