Category: Kamusi

Sehemu hii inahusu maana ya maneno ya Kiswahili na kujifunza kuhusu Lugha ya Kiswahili.

  • Maana ya neno amonia na English translation

    Maana ya neno amonia Matamshi: /amɔnia/ (Nomino katika ngeli ya [i-i]) Maana: kiowevu cha harufu kali kitumikacho kutengeneza mbolea au baruti. Amonia Katika Kiingereza (English translation) Amonia katika Kiingereza ni: ammonia. Read more

  • Maana ya neno amkua na English translation

    Maana ya neno amkua Matamshi: /amkua/ (Kitenzi elekezi) Maana: ashiria au mwambia mtu kwa sauti asogee, ajongelee au aje pale mahali ulipo. Kisawe chake ni ita. Mnyambuliko wake ni: → amkuana, amkulia, amkulika, amkuliwa. Amkua Katika Kiingereza (English translation) Amkua katika Kiingereza ni: To beckon, call or summon. Read more

  • Maana ya neno amkia na English translation

    Maana ya neno amkia Matamshi: /amkia/ Amkia 1 (Kitenzi elekezi) Maana: amkua, sabahi, salimu mtu; julia mtu hali. Mfano: Juma huwaamkia wazazi wake kila asubuhi. Mnyambuliko wake ni: → amkiana, amkika, amkilia, amkisha, amkiwa. Amkia 2 (Kitenzi si elekezi) Maana: mkesha wa; tangulia siku fulani. Mfano: Mwezi umeandama kwa hiyo kesho tutaamkia Sikuu ya Idd.… Read more

  • Maana ya neno amka na English translation

    Maana ya neno amka Matamshi: /amka/ (Kitenzi si elekezi) Maana: 1. toka kitandani au usingizini; fumbua macho. Mfano: Babake Juma amechelewa kwenda uvuvini kwa sababu hakuamka alfajiri. 2. janjaruka, zinduka, changamka au erevuka. 3. simama wima au inuka. Mfano: Mgeni wa heshima alipoingia ukumbini, watu wote waliaka na kusimama. Mnyambuliko wake ni: → amkia, amkika,… Read more

  • Maana ya neno amisa na English translation

    Maana ya neno amisa Matamshi: /amisa/ (Kitenzi elekezi) Maana: tawisha au fuga mwari au msichana pindi avunjapo ungo au kubaleghe. Mnyambuliko wake ni: → amisia, amisiana, amisika, amisana, amisiwa. Amisa Katika Kiingereza (English translation) Amisa katika Kiingereza ni: To give away or marry a girl who has reached puberty. Read more

  • Maana ya neno amirisha na English translation

    Maana ya neno amirisha Matamshi: /amirisha/ (Kitenzi elekezi) Maana: imarisha, stawisha, boresha, pea, nawirisha. Mnyambuliko wake ni: → amirishana, amirishia, amirishika, amirishiwa, amirishwa. Amirisha Katika Kiingereza  (English translation) Amirisha katika Kiingereza ni: strengthen, develop, improve. Read more

  • Maana ya neno amirika na English translation

    Maana ya neno amirika Matamshi: /amirika/ (Kitenzi si elekezi) Maana: imarika au pata uthabiti au utulivu. Mnyambuliko wake ni → amirikia, amirikika, amirikisha. Amirika Katika Kiingereza (English translation) Amirika katika Kiingereza ni: strengthen or gain stability. Read more

  • Maana ya neno amiri na English translation

    Maana ya neno amiri Matamshi: /amiri/ Wingi wa amiri ni maamiri. Amiri 1 (Nomino katika ngeli ya [a-wa]) Maana: 1. kiongozi kamanda mwenye mamlaka makubwa hasa jeshini. Kisawe chake ni jemadari. 2. mtu mwenye hatamu za mamlaka au amri. Amiri 2 (Kitenzi elekezi) Anza. Fanya kitu kwa mara ya kwanza. Amiri Katika Kiingereza (English translation)… Read more

  • Maana ya neno aminisho na English translation

    Maana ya neno aminisho Matamshi: /aminisɔ̃/ Wingi wa aminisho ni maaminisho. (Nomino katika ngeli ya [li-ya]) Maana: kabidhi mtu kitu akuwekee amana. Aminisho Katika Kiingereza (English translation) Aminisho katika Kiingereza ni: Entrustment, empowerment, or assurance. Read more

  • Maana ya neno aminisha na English translation

    Maana ya neno aminisha Matamshi: /aminisha/ (Kitenzi elekezi) Maana: 1. acha kitu au jambo chini ya mamlaka ya mtu. 2. thubutu au jasiri kufanya jambo la hatari. 3. sadikisha mtu juu ya kitu au jambo fulani. Mnyambuliko wake ni: → aminishana, aminishia, aminishika, aminishwa. Aminisha Katika Kiingereza (English translation) Aminisha katika Kiingereza inategemea na maana… Read more