Mhariri Forum

Notifications
Clear all

Ni jambo gani muhimu zaidi katika uhusiano?

   RSS

0
Topic starter

Mambo muhimu zaidi katika uhusiano ni?

4 Answers
0

Subira na uvumilivu

Kitu kimoja ambacho ni muhimu kwa uhusiano ni uvumilivu. Uvumilivu unakuwezesha kuelewana, kutatua tofauti zenu na kupendana kwa nguvu zaidi. Wakati wowote kunapotokea kutokuelewana watu huwa rahisi kuchukua uamuzi kwa hasira na kuchanganyikiwa na mara nyingi hata kuachana bila kufikiria nini kitakochotokea. Hapo ndipo uvumilivu ni muhimu. Subiri kabla ya kuamua jambo katika uhusiano. 

0
Topic starter

Mpongezi na mkosoe mwenzako. Ukizuia kumwambia mambo usiyopenda kuhusu mwenzako, basi siku moja utafunguka na hatimaye kulipuka; kusababisha chuki na uhusiano kuyumbayumba. Kumpongeza au kumkosoa husaidia mpendwa wako kuweza kujikubali na kubadilisha tabia au mazoe yake mbovu. 

0

Kujua kwamba mpenzi wako ni mzuri, anastahili kuheshimiwa, kusamehewa na kusikilizwa.

Kamwe usimdharau mwenzako. 

Kujitolea zaidi ya yote kwa ubora wa uhusiano, furaha yako mwenyewe, na furaha ya mpenzi wako.

0

Jambo muhimu zaidi katika uhusiano ni uaminifu, kwani huunda msingi wa mawasiliano wazi, kuheshimiana, na urafiki.